LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake Shinyanga wampa tuzo Rais Samia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akizungumza baada ya kukabidhiwa tuzo ya heshima na pongezi yenye alama ya namba moja kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na wanawake wa Mkoa wa Shinyanga, Jumatatu Oktoba 30,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi (kushoto) aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano la kumpongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme tuzo ya heshima na pongezi yenye alama ya namba moja kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na wanawake wa Mkoa wa Shinyanga, Jumatatu Oktoba 30, 2023.

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Wanawake Mkoa wa Shinyanga wametoa tuzo ya heshima na pongezi yenye alama ya namba moja kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo katika mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla ambapo kila kijiji kimefikiwa.

Tuzo hiyo imekabidhiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi kwa Mkuu wa Shinyanga, Christina Mndeme aliyeipokea kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akikabidhi tuzo hiyo, Samizi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kongamano la kumpongeza Rais Samia kwa kutoa fedha za kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika sekta zote ikiwemo afya, elimu maji na nishati ya umeme lililofanyika Oktoba 12, j,2023 katika Manispaa ya Shinyanga likiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, amesema tuzo hiyo ni mwendelezo wa Kongamano hilo.

“Katika kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, tuliahidi kumpa tuzo kutokana na maendeleo aliyoyaleta mkoani Shinyanga. Tumempa tuzo ya shukrani na pongezi kwa sababu amegusa vijiji vyote kwa mvua ya mabilioni ya fedha” amesema Samizi.

Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Samia, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amewashukuru wanawake mkoani humo kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Samia ya kuwaletea maendeleo wananchi.

“Naipongeza sana kamati ya maandalizi ya kongamano hili, nakiri kupokea tuzo hii yenye alama ya namba moja kutoka kwa wanawake wa mkoa wa Shinyanga na nitaifikisha kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan” amesema Mndeme na kuongeza;

“Kwa niaba ya wanawake kutoka wilaya zote za Mkoa wa Shinyanga, tunampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kuleta maendeleo mkoani Shinyanga na Tanzania kwa ujumla” ameongeza Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akionesha Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga Jumatatu Oktoba 30,2023.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akizungumza baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga Jumatatu Oktoba 30,2023.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga Jumatatu Oktoba 30,2023.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi (kushoto) ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akicheza na wanawake wakati wa akikabidhiwa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akiagana na wanawake wa mkoa wa Shinyanga baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Heshima na Pongezi yenye alama ya Namba 1 kwa ajili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan iliyotolewa na Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.