LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya Bunge yatembelea Bwawa la Membe, Nyumba za Vijana wa BBT

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mradi wa nyumba 46 za makazi ya vijana wa BBT ukiwa katika hatua mbalimbali za ukamilishaji uliopo Chinangali II jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Omari Mohamed Kiguha amesema kuwa kamati imeridhishwa na hatua za ujenzi wa mradi wa bwawa la Membe ziilizofikiwa ikilinganishwa na kiasi cha fedha zilizotolewa kwenye mradi huo.

Kiguha ameyasema hayo wakati kamati hiyo ilipotembelea mradi ikiwa ni sehemu ya mradi inayotembelewa na kamati hiyo ya Bajeti katika ziara yake ya siku nane katika mikoa mbalimbali.

Aidha katika mkoa wa Dodoma kamati imetembelea shamba la BBT la Chinangali II na kujionea hatua zilizofikiwa za ujenzi wa miundo mbinu ya nyumba za makazi ya vijana kiwanda cha mvinyo wa zabibu maandalizi ya shamba.
Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde (MB) akiongea na wananchi wa kijiji cha Membe wilayani Chamwino wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya bajeti ya bunge la Tanzania tarehe 11/11/2023.

No comments:

Powered by Blogger.