LIVE STREAM ADS

Header Ads

Fainali ya Barrick North Mara Mahusiano Cup 2023 yahitimishwa kwa kishindo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele akisaidiana na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo kukabidhi kombe kwa kapteni wa timu ya Kewanja FC, Geofrey Emmanuel, baada ya kuibuka washindi wa Barrick North Mara Mahusiano Cup 2023,baada ya kuichapa timu ya Kerende FC bao 1-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime.
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele (wa pili kulia) akikabidhi kombe kwa Kapteni wa timu ya Kewanja FC, Geofrey Emmanuel baada ya timu hiyo kuibuka washindi wa Barrick North Mara Mahusiano Cup 2023, baada ya kuichapa timu ya Kerende FC bao 1-0 katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime .Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini,Mwita Waitara na kushoto ni Meneja Mahusiano wa Barrick North Mara, Francis Uhadi.
Wachezaji wa timu za Kewanja FC na Kerende FC, wakionyeshana ubabe uwanjani wakati wa mechi ya fainali ya ligi ya Barrick North Mara Mahusiano Cup iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime.
Mabinti wakiwa tayari kutoa medali kwa ajili ya kuvisha wachezaji baada ya kumalizika kwa mechi ya fainali ya Barrick North Mara Mahusiano Cup 2023.
Mashabiki na wachezaji wa timu ya Kewanja FC wakisherehekea ushindi baada ya kuibuka kidedea katika ligi ya Barrick North Mara Mahusiano Cup iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime .
Mashabiki na wachezaji wa timu ya Kewanja FC wakisherehekea ushindi baada ya kuibuka kidedea katika ligi ya Barrick North Mara Mahusiano Cup iliyochezwa katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe wilayani Tarime.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mechi hiyo ya fainali.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mechi hiyo ya fainali.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mechi hiyo ya fainali.
Viongozi wa wilaya ya Tarime wakiingia uwanjani kushuhudia mechi hiyo.
Baadhi ya wachezaji walioshiriki ligi hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na Rais na Afisa Mtendaji wa Barrick, Mark Bristow (nyuma aliyevaa kofia) wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo mwezi Septemba mwaka huu.


***
Mechi ya fainali ya soka ya ligi ya soka ya Barrick North Mara Mahusiano Cup, ilichezwa mwishoni mwa wiki katika uwanja wa shule ya sekondari ya Ingwe iliyopo katika kitongoji cha Nyamongo wilayani Tarime, ambapo timu ya Kewanja FC iliichapa Kerende FC bao 1-0 na kutetea ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya tatu mfululizo.

Mashindano ya Mahusiano Cup 2023, yalizinduliwa kwenye uwanja huo huo Septemba 29, mwaka huu na Rais na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Barrick, Mark Bristow. Yakiwa na Kaulimbiu isemayo “Mahusiano Bora kwa Uwekezaji Endelevu”.

Mgeni rasmi katika fainali hiyo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mtenjele, ambaye alikabidhi zawadi ya kombe na fedha taslimu kwa timu ya Kewanja FC, na zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi wa pili (Kerende FC) na wa tatu (Mrito FC).

Wengine waliopata zawadi ya fedha taslimu ni mwamuzi bora, Jacob Odongo, kocha bora, mchezaji bora, kipa bora, timu iliyoonesha nidhamu na mtangazaji bora wa mashindano hayo, Frank Jackson Chacha.

Mechi ya fainali ya mashindano hayo ilifana na kuwa kivutio kikubwa kutokana na kuhudhuriwa na mamia ya wananchi kutoka vijiji na kata zinazozunguka mgodi wa Barrick North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, Mara.

Viongozi wengine waliohudhuria fainali hiyo ni Meneja Mahusiano wa Mgodi wa Baarick North Mara, Francis Uhadi aliyemwakilisha Meneja Mkuu wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko, na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ulipo mgodi wa North Mara, Solomon Shati na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Gimbana Ntavyo.

Wakati huo huo mashindano hayo yamewezesha upatikanaji wa wachezaji 37 watakaounda timu mpya itakayoitwa North Mara FC.

Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano Mahusiano Cup, Mwita Marwa Magige, alisema wachezaji 37 walioteuliwa kuunda timu ya North Mara FC ni wale ambao wameonesha ubora na vipaji mahiri katika mashindano hayo.

Mwita, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nyamwaga alisema wachezaji hao wakiwemo magolikipa watatu wameteuliwa kutoka timu mbalimbali zilizoshiriki mashindano hayo.

No comments:

Powered by Blogger.