LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la SEMA yakabidhi miradi ya zaidi ya shilingi Bilioni nne

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga akizungumza Novemba 22, 2023 wakati akifungua kikao cha kupokea miradi sita iliyotekelezwa katika Wilaya tatu mkoani Singida na Shirika lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA) kwa kushirikiana na Shirika la Stromme Foundation . Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Sema, Ivo Manyaku na Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Singida, Romwald Mwendi.


Na Dotto Mwaibale, Singida
Shirika lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA) limekabidhi kwa Serikali ya Mkoa wa Singida miradi sita ambayo ilikuwa ikiitekeleza kwenye Halmashauri tatu za Wilaya ya Iramba, Ikungi na Manyoni ili ziiendeleze kuisimamia baada ya shirika hilo kumaliza miaka mitano ya utekelezaji ambao utafikia tamati Desemba 31, 2023.

Miradi hiyo ambayo ni ya kimtambuka ilikuwa ikitekelezwa na shirika hilo kuanzia mwaka 2019- 2023 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Stromme Foundation ambayo iligharimu zaidi ya Sh.Bilioni 4.5 kuitekeleza.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Ivo Manyaku akizungumza Novemba 22, 2023 katika kikao cha kukabidhi miradi hiyo kwa Serikali, aliitaja miradi iliyotekelezwa katika kipindi hicho ni pamoja na uwezeshaji jamii kiuchumi, mradi wa kuweka akiba na kukopa (WEKEZA), mradi wa Bonga (NJOO TUONGEE), mradi wa elimu ya mafunzo ya ufundi kwa vijana (TUNAWEZA), mradi wa elimu ya awali na makuzi, mradi wa Kuzijengea uwezo asasi za kiraia na mradi wa uwezeshaji jamii Kilimo biashara.

Alisema miradi hiyo imewanufaisha watu takribani 450,000 ambayo ililenga kukabiliana na wimbi kubwa la umasikini kwenye makundi ya jamii, likiwemo kundi la vijana, wasichana na watu wenye mahitaji maalumu.

Manyaku alitaja malengo mengine ya miradi hiyo ilikuwa ni kuboresha uchumi kwa walengwa, afya na lishe, elimu jumuishi, huduma ya maji na usafi wa mazingira, utawala bora, kilimo na mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dkt. Fatma Mganga ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kikao hicho, Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali Watu, Stephen, Pancras aliwataka maafisa maendeleo ya jamii wa halmashauri za wilaya mkoani hapa kuhakikisha wanawahamasisha wananchi kujiunga kwenye vikundi ili idadi ya wanufaika wa miradi hiyo iwe kubwa kwa kuzingatia kuwa kupitia vikundi hivyo ndimo yanamopatikana maendeleo.

Pancras alipongeza juhudi kubwa za wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapa likiwamo shirika la Sema na Stromme Foundation ambayo kwa kiwango kikubwa yameleta tija na ustawi wa maisha kwa wana-Singida.

“Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika haya na mengine na wadau wa maendeleo mtakao jitokeza lengo ni kuhakikisha mnaisaidia jamii,” alisema Pancras.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Singida Dkt. Elpidius Baganda alilipongeza shirika hilo kwa kutekeleza miradi ya sekta ya elimu na kuwa elimu ikitolewa sawa sawa ndio suluhisho la mambo mengi katika maisha ya wanadamu.

Aidha Baganda alitumia nafasi hiyo kuipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi ambayo yanayafanya mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali kutekeleza miradi yao pasipo bughudha zozote.

Baadhi ya viongozi na maafisa maendeleo ya jamii wanaosimamia na kukagua miradi hiyo waliohudhuria kikao hicho walilipongeza Shirika la Sema kwa kuwa kinara mkoani hapa katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa viwango vya juu na thamani halisi inayolingana na fedha zilizotolewa na wafadhili.

Shirika la Sema ni Shirika lisilokuwa la Kiserikali lililosajiliwa Machi 10,1998 na kuanza rasmi shughuli za utekelezaji Januari 1,2000 na lilipata hati ya ukubalifu (Certificate of Compliance) Machi 9, 2006 na makao yake makuu yapo Manispaa ya Singida eneo la Utemini (Mtaa wa Viwanda).
Katibu Tawala Msaidizi, Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Singida, Stephen Pancras (katikati), akizungumza wakati akiongoza kikao hicho..
Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa wa Singida, Romwald Mwendi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu Mkoa Singida Dkt. Elpidius Baganda akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu- Divisheni ya Elimu ya Awali na Msingi Wilaya ya Iramba, Rose Willgeofrey Kibakaya akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Elimu Watu Wazima Mkoa wa Singida, Sarah Mkumbo akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Sema, Ivo Manyaku, akizungumzia kuhusu mradi huo.
Kikao kikiendelea.
Wafanyakazi wa Shirika la Sema wakiwa kwenye kikao hicho.
Afisa ufuatiliaji na Tathmini wa Sema, Daniel Chacha ambaye alikuwa mshereheshaji akiongoza kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Meneja Miradi wa Sema, Rachel Sedute, akitoa taarifa ya miradi hiyo.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Sema, Emmanuel Hamisi akitoa taarifa ya miradi hiyo.
Afisa Umwagiliaji, Kilimo na Ushirika Wilaya Ikungi, Gurisha Msema akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Halmashauri za Iramba, Ikungi na Manyoni zinazotekeleza mradi huo wakiwa kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala Msaidizi, Usimamizi, Ufuatiliaji na Ukaguzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Shabani Mongomongo akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Iramba Omari Lanjui akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Singida, Stanslaus Choaji akizungumza.
Viongozi meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja Ma maafisa maendeleo kutoka katika wilaya za Iramba, Ikungi na Manyoni ulipotekelezwa mradi huo.
Viongozi wa meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Sema.
Picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Sema.

No comments:

Powered by Blogger.