LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yamwaga vifaa tiba mkoani Singida

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (katikati kulia) akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu ikiwa ni ishara ya kumkabidhi jenereta na vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali kupitia MSD katika hafla iliyofanyika Novemba 20, 2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi.



Na Dotto Mwaibale, Singida
Serikali  ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Bohari ya Dawa (MSD) imekabidhi vifaa tiba Mkoa wa Singida vyenye jumla ya takribani Sh.Milioni 222.472.

Vifaa hivyo ni pamoja na majenereta, sambamba na vifaa vitakavyotumika kuhudumia watoto wanaozaliwa kabla ya muda na huduma nyinginezo ambavyo vimekabidhiwa kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Kituo cha Afya Sepuka na Hospitali ya Wilaya ya Singida, Ilongero.

Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo ambayo ilishuhudiwa na wabunge, watendaji wa idara mbalimbali za sekta ya afya, wananchi pamoja na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Meneja wa MSD Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa amrsema kazi hiyo ya usambazaji wa vifaa hivyo ni jukumu lao walilopewa na Serikali.

" Kazi yetu kubwa sisi MSD ni Uzalishaji, Ununuzi,  Uhifadhi na Usambazaji wa  bidhaa za Afya na vitendanishi hapa nchini ambayo tunaifanya kwa mamlaka ya kisheria," alisema Jumaa.

"MSD tupo hapa Ikungi kukabidhi jenereta, kitanda cha kufanyia upasuaji, Ultra-Sound mashine pamoja na mashine ya kusaidia kuwapatia joto watoto wachanga na waliozaliwa kabla ya wakati
.(njiti- Infant Radlant warmer) vyenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 72".

Jumaa amesema lengo kubwa la kupelekwa kwa vifaa hivyo ni kuhakikisha huduma za uzazi zinaboreshwa na kuwa katika wilaya hiyo MSD ilikuwa inakamilisha vifaa ambavyo ilikuwa imepokea fedha zaidi ya Sh. Milioni 300 ili kukamilisha usambaji wake.

Alisema MSD Kanda ya Dodoma imepokea maombi  ya vifaa  tiba zaidi ya  700  Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa ajili ya vituo  vya Afya  na Zahanati.

"Ukiangalia muda tuliopokea fedha hizi na utekelezaji wa kupeleka vifaa hivyo ni muda mfupi sana na hiyo imetokana na Serikali kuboresha huduma za MSD na kufikia hatua hii ya kukamilisha vifaa ambavyo hatukuvipeleka awali na kuvipeleka sasa baada ya fedha zake kuzipokea muda mfupi uliopita" amesema Jumaa.

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha na MSD imekuwa ikinunua na kusambaza vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya kote nchini ambapo aliishukuru kwa hatua hiyo na kueleza kuwa inajenga morali kwa watumishi wa sekta ya afya na kuipenda kazi wanayoifanya.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameishuru Serikali na MSD kwa kupeleka vifaa hivyo na kueleza kuwa sekta ya afya ni uhai na kuwa watu wakiwa na afya njema ndipo wataweza kufanya kazi zao vizuri.

"Leo hii tunashuhudia vifaa hivi vilivyo letwa na Serikali kupitia MSD na kukabidhi hospitali yetu ya Ikungi maana yake ni utekelezaji wetu wa kujenga Hospitali ya Wilaya ambayo tuliiomba kwa muda mrefu" amesema Mtaturu.

Amesema kujenga majengo tu ya hospitali haitoshi na kuwa inahitaji na vitu vya ziada vikiwemo vifaa na kuwa madaktari na wataalamu wengine wamesomeshwa kwa lengo la kuwasaidia watu kutibu maradhi mbalimbali na kwa kuvitumia vifaa hivyo ndio wanaweza kufanya kazi yao kwa urahisi iwe kwa kupima na kufanya upasuaji.

Mtaturu amesema Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mapinduzi makubwa sana katika sekta ya afya hapa nchini hivyo kila mtu mpenda maendeleo anapaswa kumshukuru kwa jinsi anavyo iendesha nchi kwenye sekta mbalimbali.

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akipokea vifaa hivyo kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Sepuka amesema miongoni mwa vifaa alivyo pokea kutoka MSD ni jenereta lenye ukubwa wa KVA 60 na vifaa vingine 11 ambavyo baadhi ni toroli la kuwekea vifaa wakati madaktari na wauguzi wanapokwenda kutoa huduma, vifaa vinavyotumika kumsaidia mtoto baada ya kuzaliwa aweze kupumua vizuri na kuwa vifaa vyote alivyovipokea vinatumika kupingana na uzazi pingamizi na lengo lake ni kumuokoa mama wala mtoto wasife wakati wa kujifungua.

Ametaja vifaa vingine alivyopokea ni mashine kwa ajili ya hewa, mashine ya kupimia uzito, kifaa cha kutundikia dripu ya maji, kifaa cha kuwapa joto watoto waliozaliwa kabla ya muda, kifaa cha kuvuta uchafu kwenye njia ya hewa baada ya mtoto kuzaliwa, saa ya ukutani, kifaa kinachobeba vifaa vya kumuhudumia mtu aliyepata majeraha na pampu inayotumika kumnyonya mtoto kwa ajili ya kuondoa kitu kilichokwama kooni au kupoteza fahamu baada ya kupaliwa na kuwa vifaa hivyo vyote vina thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 82.

Kingu ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha na akapongeza maboresho makubwa yaliyofanywa ndani ya MSD na kueleza kuwa MSD ya leo ni ya kisasa na mkombozi kwa wananchi katika kazi ya kutoa huduma za afya si kwa Mkoa wa Singida pekee bali kwa nchi nzima kazi ambazo zimekuwa zikionekana kupitia vyombo vya habari.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo ameishukuru Serikali kwa kuwapelekea jenereta na gari la kuwabebea wagonjwa na wajawazito ambao wengi wao walikuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa umeme wa uhakika wakati wakipata huduma hasa za upasuaji na kukosekana kwa gari la kuwapeleka hosptali wanapokuwa wagonjwa.

Ighondo amesema pamoja na kupelekewa gari hilo pia Serikali kupitia MSD imewapelekea kifaa kinachotumika kwa ajili ya kuwaongezea joto watoto wanaozaliwa chini ya muda.

Amesema mbali ya gari hilo la wagonjwa vifaa walivyopokea vina thamani ya zaidi ya Sh.Milioni 62.7

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Dorisila Mlenga, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Singida Grace Ntogwisangu na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Sepuka Kesia Daniel wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea vifaa hivyo ambavyo vinakwenda kuwarahisishia utendaji wa kazi za kutoa huduma kwa wananchi ambapo wamesema watavisimamia na kuvitunza ili viweze kudumu kwa muda mrefu wakizingatia Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuvinunua.

Wananchi Elesisia Mlenga, Asha Salim, Asha Musa, Mwalimu Tatu Njoka, Ashura Iddi na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Seketoure, Getruda Yona wameishukuru Serikali kupitia MSD kwa kuwapekea jenereta na gari la wagonjwa na kueleza kuwa vifaa hivyo vinakwenda kuwasaidia katika kupata huduma bora za afya.

Mwanafunzi Getruda Yona amemshukuru Rais Samia kwa kuwajengea shule na kuwapunguzia umbali mrefu ambapo walikuwa wakitembea zaidi ya kilomita 10 kwenda shuleni kabla ya kujengewa kwa shule hiyo ya Seketoure.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (katikati kulia) akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu ikiwa ni ishara ya kumkabidhi jenereta na vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali kupitia MSD katika hafla iliyofanyika Novemba 20,2023 katika Kituo cha Afya cha Sepuka Wilaya ya Ikungi. Kutoka kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Sepuka, Kesia Daniel, Diwani wa Kata ya Sepuka Halima Ng'imba, Afisa Huduma Mwandamizi kwa Wateja MSD Kanda ya Kati, Juliana Mbogo na Mfamasia wa Kanda na Afisa Huduma kwa Wateja MSD Kanda ya Kati Dodoma, Michael Mwakuna.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (katikati kushoto) akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo ikiwa ni ishara ya kumkabidhi jenereta na vifaa tiba vilivyotolewa na Serikali kupitia MSD katika hafla iliyofanyika Novemba 20,2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Singida.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (katikati kulia) akisisitiza jambo wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa Mbunge wa Jimbo la Singida, Magharibi Elibariki Kingu (kushoto) Kulia ni Afisa Huduma kwa Wateja Mwandamizi wa MSD Kanda ya Kati, Juliana Mbogo.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa, akipeana mkono na Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Sepuka Kesia Daniel baada ya kukabidhi vifaa hivyo.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa, akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa MSD na wakituo cha Afya cha Sepuka baada ya kukabidhi vifaa tiba hivyo.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa, akizungumza na wakazi wa Wilaya ya Singida wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
Mbunge Ramadhani Ighondo akizungumza na wananchi wakati wa hafla hiyo.
Mganga wa Wilaya ya Singida, Grace Ntogwisangu, akizungumza na wananchi kwenye hafla hiyo.
Gari la MSD , likiwa tayari kushusha vifaa hivyo.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa (katikati) na Afisa Huduma Mwandamizi kwa Wateja wa NSD, Juliana Mbogo wakiwajibika wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu, akizungumza na wananchi wa Kata ya Sepuka wakati wa kupokea vifaa hivyo.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu,Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa na Afisa Huduma Mwandamizi kwa Wateja wa MSD, Juliana Mbogo wakiwa na zawadi zao za kuku walizopewa na Wanawake wa Kata ya Sepuka.
Wananchi wa Kata ya Sepuka wakiwa kwenye hafla ya kupokea vifaa hivyo.
Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Dodoma Mwanashehe Jumaa, akiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliohudhuria kliniki wakati wa makabidhiano ya vifaa hvyo Kata ya Sepuka.
Muonekana wa moja ya magenereta yaliyo kabidhiwa na MSD katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi, Singida na Kituo cha Afya cha Sepuka.
Wanawake wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa vifaa hivyo Hospitali ya Wilaya ya Singida, Ilongero.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Seketoure wakiwa kwenye hafla hiyo.
Diwani wa Kata ya Ilongero, Issa Mwiru akizungumza na wananchi wakati wa hafla hiyo.
Gari la wagonjwa lililotolewa na Seerikali kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Singida likioneshwa kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo ya kupokea vifaa tiba.
Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Ilongero, Mwanamoshi Bakari, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Hosptali ya Wilaya ya Ikungi.
Muonekano wa moja la jengo la Kituo cha Afya cha Sepuka.
Muonekano wa moja ya jengo la Hospitali ya Wilaya ya Singida Ilongero.
Jenereta likiwa limebebwa kwa jeki tayari ya kuhifadhi katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi wakati ikisubiriwa kujenga kibanda litakalo wekwa.

No comments:

Powered by Blogger.