LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya Naweza Tena yatoa msaada kwa waraibu wa dawa za kulevya Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Taasisi ya Naweza Tena inayowasaidia waraibu wa dawa za kulevya jijini Mwanza imekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali kwa baadhi ya waraibu wanaopata tiba ya methadoni katika Hospitali ya Sekou Toure.

Akizungumza jumamosi Disemba 23, 2023 wakati wa zoezi la kukabidhi msaada huo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Esther Morris amesema lengo ni kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya kufurahia sikukuu ya Christmas kama wana jamii wengine.

Morris ambaye pia ni Mkurugenzi wa Millagro Car Wash iliyopo Mission jijini Mwanza ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa jamii kuwasaidia waraibu wa dawa za kulevya kuondokana na changamoto ya kutumia dawa hizo.

Amesema jamii isipowasaidia ni rahisi waraibu hao kushawishika kurejea kwenye matumizi ya dawa za kulevya ambapo ameshauri wadau mbalimbali kutoa kazi zisizohitaji ujuzi ili kuwasaidia kujipatia kipato hatua itakayosaidia kutojihusisha na mtukio ya maovu ikiwemo udokozi.

Morris pia amewashukuru wadau wote waliofanikisha upatikanaji wa msaada huo ambao ni pamoja mamlaka ya kupambana na kudhubiti dawa za kulevya nchini (DCEA), Mkurugenzi wa kampuni ya CMG/ Nyanza Bottle- Christopher Gachuma, Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, taasisi ya Teens Corridor, kampuni ya Zongii Plumbing na familia ya Dokta Temba.

Nao baadhi ya waliopokea msaada huo, Meris Mabula na Emmanuel Betty wameshukuru kwa msaada huo na kuahidi kuwa mabalozi wema katika jamii kwa kuhamasisha wenzao kuacha matumizi ya dawa za kulevya huku wakiomba wadau wengine kupiga mfano wa taasisi ya Naweza Tena ambayo imekuwa ikiwasaidia mara kwa mara.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa taasisi ya Naweza Tena na Millagro Car Wash, Esther Morris akizungumza wakati wa zoezi la kutoa msaada wa chakula kwa waraibu wa dawa za kulevya jijini Mwanza kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Christmas, Disemba 25, 2023.
Zoezi la kukabidhi msaada wa vyakula kwa waraibu wa dawa za kulevya.
Zoezi la kukabidhi viatu likiendelea.
Taasisi ya Youth VDT iliyopo Manispaa ya Ilemelea mkoani Mwanza imesaidia upatikanaji wa viatu kwa waraibu hao.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> kuhusu Naweza Tena

No comments:

Powered by Blogger.