LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Shinyanga akabidhi msaada Hanang' Manyara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akionesha misaada ya kibinadamu iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akikabidhi sehemu ya nguo zilizotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akionesha misaada ya kibinadamu iliyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amekabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.

Mndeme akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita amekabidhi misaada hiyo Desemba 22, 2023 kwa Mkuu wa wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja.

Akizungumza wakati wa kukabidhi misaada hiyo, Mndeme amesema WanaShinyanga wanaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kutokana na janga lililotokea Hanang lililosababishwa mvua kubwa iliyoambana na tope, mawe na miti hivyo kupelekea vifo, mali kupotea, mifugo kufa, mashamba kuharibika, nyumba kuharibika.
"Sisi wana Shinyanga tukiwa sehemu ya Watanzania tulipoguswa na janga hili tulipokea kwa masikitiko makubwa, baada ya kupokea taarifa hii ya kusikitisha, wanashinyanga kwa mapenzi mema wakaona nao wamuunge mkono Mhe.  Rais Samia Suluhu Hassan lakini vile vile wawaunge mkono wananchi wengine kutoa pole kwa wananchi wa Hanang hivyo tumefika hapa katika mji huu wa Katesh kuwasilisha kwako mhe. DC pole zetu ili kuonesha mshikamano, umoja na kwamba tuko pamoja katika kipindi hiki kigumu ambapo kwa wenzetu wa Hanang wanapitia" amesema Mndeme.

"Kwa niaba ya wananchi wa Shinyanga ambao wamejitolea kutoa pole zao kwa ndugu zao wa Hanang, naomba nikakibidhi mifuko 1000 ya saruji, mchele kilo 700, unga wa mahindi kilo 355, unga lishe kilo 250,juisi katoni 500, chumvi pakti 90, sukari kilo 25,sabuni katoni 13,mafuta ya kula lita 5, viatu pea 43, nguo balo 30 kati ya balo hizo 27 zina nguo za wanaume na tatu nguo mchanganyiko” amesema
“Misaada hii inatoka kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga ambao wamejitolea kwa mapenzi yao mema, wameguswa kwa namna moja au nyingine. Poleni sana wan Hanang, pole sana Rais Samia, tuendelee kumuomba Mungu atuepushe na majanga haya, mvua tunaihitaji, tunaumuomba Mungu atuletee mvua yenye neema. Msaada tuliotoa ni mdogo ukilinganisha na madhara yaliyotokea tunaomba hiki kilichotolewa na wana Shinyanga mkipokee” ameongeza Mndeme.

Akipokea misaada hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Janeth Mayanja amewashukuru Wana Shinyanga kwa upendo,huruma, utu, ubinadamu na undugu wa kweli waliouonesha kwa wan Hanang akisisitiza pia wamemuunga mkono kwa vitendo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Tunawashukuru sana Wana Shinyanga kwa misaada ya kibinadamu mliyotupatia, mmeongeza nguvu Hanang na vifaa hivi vya ujenzi mlivyotoa vitasaidia katika ujenzi wa makazi ya waathirika wa janga lililotokea” amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme (kulia) akimpa pole Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, Janeth Mayanja kufuatia janga la mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka Mlima Hanang'.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika Wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akikabidhi sehemu ya nguo zilizotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi, katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga
Mkuu wa Wilaya ya Hanang mkoani Manyara, Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, Janeth Mayanja akitoa neno la shukrani kwa wananchi wa Shinyanga.
 Awali Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi, (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita wakikagua mzigo walioleta Hanang'.
Mwonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Mwonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Mwonekano wa magari yaliyobeba misaada ya kibinadamu ikiwemo chakula, nguo na vifaa vya ujenzi vilivyotolewa na wananchi wa Shinyanga kwa waathirika wa mafuriko ya tope yaliyoambatana na mawe kutoka mlima Hanang' katika wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi  (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita wakitembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'.
Katibu Tawala Wilaya ya Hanang', Mwl. Athuman Likeyekeye akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita walipotembelea moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme( katikati) Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi  (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita wakiwa katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akiangalia miongoni mwa mawe yaliyosukumwa na maji kutoka mlima Hanang' hadi katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme akiangalia miongoni mwa miti iliyosukumwa na maji kutoka mlima Hanang' hadi katika eneo la Jorodom moja ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko wilaya ya Hanang'.

No comments:

Powered by Blogger.