LIVE STREAM ADS

Header Ads

MPC yakemea waandishi wa habari kusifia nyama ya mbunge

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
TAARIFA  KWA UMMA  JUU  YA  UVUNJIFU WA  MAADILI  YA  UANDISHI WA  HABARI.

Klabu  ya  Waandishi wa Habari ya  Mkoa wa Mwanza (MPC), ni  klabu   iliyosajiliwa  kwa  sheria  ya Society  Act Mwaka  1994 na kupewa namba  ya  usajili ya  SO 8262, ikiwa  na  dhima  kuu  ya  kusimamia  weledi wa uandishi wa habari  ndani  ya  Mkoa wa Mwanza.
 
MPC  imefuatilia kwa  ukaribu  kusambaa  kwa  kipande cha  picha  nyongefu  kikionesha  Mwandishi wa Habari  Emmanuel  Twimanye   akimshukuru  Hamisi  Mwagao  Tabasamu Mbunge  wa  Jimbo  la  Sengerema   kwa  kutoa  mgao wa  nyama  ya  Mbuzi na Kondoo  kwa   baadhi  ya  waandishi wa  habari wa  Wilayani  Sengerema, Mkoa wa Mwanza, tukio  lililotokea  Januari 1, 2024.
 
MPC inalaani  kitendo  hicho  kwa  kuwa,  kinakiuka misingi   na maadili   ya  uandishi wa  habari  kwani Mwandishi wa  Habari  hatakiwi  kupokea  pesa,  zawadi   au  bakishishi   yoyote  ile  kutoka  kwa Mwanasiasa, Afisa wa  Serikali au Mfanyabiashara ili  kuepuka  mgongano  wa  kimaslahi  kwenye  utendaji  kazi  wake.
 
MPC inalaani kitendo  hicho na  imechukua  hatua   za kuwaonya  waandishi  wote  waliohusika  kwenye  tukio  hilo na kuwaelimisha athari za vitendo  hivyo  kwenye  tasnia  ya  habari  na mtazamo  wa jamii  na inawataka  waandishi  wote  kuzingatia  maadili  ya  uandishi wa  habari kuelekea  kwenye  uchaguzi wa Serikali za Mitaa  2024  na  uchaguzi  Mkuu wa Mwaka  2025.
 Edwin Soko
 Mwenyekiti
 MPC
 02.01.2024


No comments:

Powered by Blogger.