MWANZA: Mshindi wa Tisha na Tembo Card akabidhiwa zawadi nono
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imekabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya ‘Tisha na Tembo Card- Tukakiwashe AFCON’ kwa mwezi Disemba mwaka 2023, aliyetokea jijini Mwanza.
Hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi huyo imefanyika Jumatano Januari 17, 20234 katika benki ya CRDB tawi la Mwanza.
Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta amesema kampeni hiyo ilianza mwezi Novemba 2023 na itafikia tamati Februari 02, 2024 ambapo watumiaji wa ‘Tembo Card’ watajishindia fedha taslimu, samani za nyumbani na vifaa vya kielekroniki.
Pia amesema washindi wanane wataenda nchini Ivory Coast kushuhudia michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) ambapo tayari wateja wanne wamelipiwa gharama zote kwenda kushuhudia michuano hiyo.
“Washindi wanane wataenda kuangalia mashindano ya AFCON, mshindi mmoja atapata milioni moja, washindi wawili watapata laki tano kila mmoja. Tayari mshindi wa mwezi Novemba 2023 kutoka Tanga amekabidhiwa zawadi ya seti ya sofa na leo tuko hapa kumkabidhi zawadi mshindi wa mwezi Disemba 2023 aliyeshinda vifaa vya kisasa vya kielekroniki” amesema Sitta.
Sitta amemtaja mshindi huyo kuwa ni Marion Albert Cesari kutoka jijini Mwanza ambaye amejishindia zawadi zenye thamani ya shilingi milioni tisa ambazo ni runinga nchi 75 (milioni 2.6), jokofu (milioni 4.2) na redio (milioni 2.2) na kutoa rai kwa wateja wengine wa CRDB kuendelea kufanya malipo ya bidhaa mbalimbali kwa Tembo Card ili kupata nafasi zaidi ya kujishindia zawadi.
Naye mshindi huyo, Marion Cesari amesema amekuwa na desturi ya kutumia Tembo Card kufanya malipo ya bidhaa mbalimbali ikiwemo ya mtandaoni hatua ambayo ilimuongezea nafasi ya kuibuka mshindi na hivyo kuwahimiza wateja wengine kutumia huduma hiyo badala ya kutembea na fedha mfukoni kwa ajili ya malipo.
"Nitumie hadhira hii kuwahamasisha watanzania wote kuhakikisha wanatumia kazi zao ili wawe na nafasi ya kushinda kwenye zawadi ijayo mwisho wa mwezi huu wa Januari, pia nitoe rai kwamba chaguo sahihi la benki ni CRDB, unafanya malipo yako lakini inakuzawadia" amesema Kaimu Mkuu Kitengo cha Kadi CRDB, Karington Chahe.
Awali akikabidhi zawadi kwa mshindi huyo, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya amewahimiza wananchi kuhamasika kutumia huduma za kibenki ikiwemo mikopo inayotolewa na CRDB ili kukuza zaidi shughuli zao za kimaendeleo.
“Dada yetu Marion amefungua pazia la washindi wa zawadi za kampeni ya Tisha na Tembo Card kwa Mkoa wetu wa Mwanza, nichukue nafasi hii kumpongeza kwa zawadi hizi ambazo zitabadili mwonekano wa sebure yake” amesema Balandya akiwahimiza wananchi kutumia huduma za kibeki.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya (kulia) akizungumza wakati wa kumkabidhi zawadi mshindi wa kampeni ya Tisha na Tembo Card kwa mwezi Disemba 2023 ambaye ni Marion Cesari (wa pili kulia). Wa kwanza kushoto ni Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sita na anayefuata ni Kaimu Mkuu Kitengo cha Kadi CRDB, Karington Chahe.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa Tisha na Tembo Card, Tukakiwashe AFCON kwa mwezi Disemba 2023, Marion Cesari. Kushoto ni Kaimu Mkuu Kitengo cha Kadi CRDB, Karington Chahe na wa pili kulia ni Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta.
Mshindi wa Tisha na Tembo Card, Tukakiwashe AFCON kwa mwezi Disemba 2023, Marion Cesari akitoa shukurani baada ya kukabidhiwa zaidi na benki ya CRDB jijini Mwanza.
Huduma ya Tembo Card ilizinduliwa na benki ya CRDB mwaka 2002 ikianza kutumika kwa matawi ya Tanzania na mwaka 2004 iliungana na kampuni ya Visa Card na kuwawezesha wateja wake zaidi ya milioni nne nchini kupata huduma ya kifedha kote duniani kupitia mashine za ATM na POS.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: