LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waratibu programu ya kizazi chenye usawa watakiwa kuwa wabunifu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini wametakiwa kubuni mikakati madhubuti itakayosaidia kutekeleza kwa ufanisi programu ya ahadi za nchi katika kizazi chenye usawa katika maeneo yao.

Rai hiyo imetolewa Januari 16, 2024 na Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya wakati akihitimisha mafunzo ya siku mbili kwa maafisa maendeleo ya jamii kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju.

Amesema baada ya mafunzo hayo ni vyema washiriki hao wakasaidia utekelezaji wa programu hiyo kwa ufanisi ikiwemo Halmashauri kuzingatia maandalizi ya bajeti yenye mrengo wa kijinsia.

“Mikakati ambayo mmeiandaa kupitia mafunzo haya ikiwemo mbinu za mawasiliano, mkaitekeleze kikamilifu na kutoa taarifa ya utekelezaji kwa wakati hatua itakayosaidia kuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia” amesema Balandya.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia na wanawake kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Juliana Kibonde amesema program ya kizazi chenye usawa ina malengo mbalimbali ya utekelezaji ambapo Tanzania ilichagua eneo la haki na usawa kiuchumi ambapo watekelezaji ni maafisa maendeleo ya jamii.

“Sisi kama nchi, mama yetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alichagua eneo la haki ya usawa wa kiuchumi ambapo katika mafunzo haya tumewaelimisha jinsi ya kuandaa taarifa za msingi kuhusu utekelezaji wa masuala ya usawa wa kijinsia na uchumi ili tuweze kujipima” amesema Kobonde.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tabora, Panin Kerika amesema mafunzo hayo yamewakumusha wajibu wao na yamekuwa chachu ya kufanya kazi kwa weledi.

Mafunzo hayo ya awamu ya pili yamefanyika jijini Mwanza kwa muda wa siku mbili Januari 16 na 17, 2024 yakiwashirikisha maafisa maendeleo ya jamii kutoka Mikoa 15 ya Tanzania Bara, ambapo katika awamu ya kwanza mafunzo kama hayo yalifanyika jijini Dar es salaam yakijumuisha washiriki kutoka mikoa 11 na hivyo kukamilisha jumla ya mikoa yote 26 na halmashauri zake 184 kote Tanzania Bara.
Na WMJJWM, Mwanza
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya akihitimisha mafunzo kwa maafisa maendeleo ya jamii kutoka mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa, Manyara, Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida, Tabora.
Maafisa maendeleo ya jamii wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya wakati akihitimisha mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo kuhusu utekelezaji wa programu ya kizazi chenye usawa.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Jinsia na wanawake kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum- Juliana Kibonde akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo jijini Mwanza.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

No comments:

Powered by Blogger.