Wenje apita Mtaa kwa Mtaa jijini Mwanza kuhamasisha maandamano
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Ezekiel Wenje amekutana na makundi mbalimbali wakiwemo machinga, bodaboda na wajasiriamali katika masoko na kuwahamasisha kushiriki maandamano ya amani yaliyoandaliwa na chama hicho yanayotarajiwa kufanyika Jumatano Februari 15, 2024 jijini Mwanza.
Wenje ambaye pia alikuwa mbunge wa Jimbo la Nyamagana kwa mwaka 2010/2015 amesema wananchi wanapaswa kushiriki maandamano hayo ili kufikisha kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Maandamano hayo yataanzia katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza na kuhitimishwa katika uwanja wa Furahisha ambapo viongozi mbalimbali wa CHADEMA wataongea na wananchi.
Tazama BMG ONLINE TV hapa chini
No comments: