LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mradi wa IMARISHA JAMII watambulishwa mkoani Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Dignity and Wellbeing for Women Living with HIV in Tanzania (DWWT) tarehe 18/03/2024 limeutambulisha mradi wa IMARISHA JAMII utakaotekelezwa katika wilaya za Buchosa, Ukerewe na Magu.

Kwa mujibu wa mratibu wa mradi huo, Bahati Haule amesema mradi huo umelenga kutoa huduma kamili za kuzuia maambukizi ya VVU ikiwemo kuzuia maambukizi,kuunganisha na kuwabakisha watu kwenye huduma zinazohusiana na VVU.

Akizungumzia makundi yatakayoguswa na mradi huo Bahati amesema ni wasichana balehe, wanawake vijana, wavuvi na jamii inayowazunguka pamoja na wale wanaofanya biashara za ngono.
Bahati Haule, Mratibu wa Mradi.
Erica Steven Mratibu wa Kudhibiti UKIMWI Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.