LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwanachama wa TALWGU auawa kwa mkuki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu mkuu TALGWU, Rashid M. Mtima
***


Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Tanzania (TALGWU) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mwanachama na kiongozi wetu, Madadi Omari Litumbui aliyekuwa Mtendaji wa Kijiji cha Mtumbei Mpopela Kata ya Kandawale Tarafa ya Kipatimu Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.

Aidha mpaka umauti unamfika Ndg. Madadi Omari Litumbui alikuwa anahudumu TALGWU kwa nafasi ya Katibu wa Kamati ya Uratibu Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa

Kifo cha Mwanachama wetu kimetokea tarehe 17 Machi 2024 ambapo alichomwa mkuki na Wafugaji (Wamang'ati) na aliwahishwa Kituo cha Afya Nanjilinji (Kilwa) lakini alifariki usiku huohuo wa tarehe 17/03/2024.

Tukio hilo lilitokea pindi marehemu Madadi Omar Litumbui anatekeleza majukumu yake kama Mtendaji wa Kíjiji ambapo alikuwa na wenzake katika doria ya hifadhi ya msitu wa Serikali uliounganisha Vijiji na kuwa hifadhi moja ambapo wakati wanawaondoa wafugaji (Wamang'ati) katika hifadhi hiyo ndipo wafugaji hao waliporusha mkuki uliomchoma Madadi na kupelekea kifo chake.

TALGWU inalaani vikali mauaji ya Mwanachama wetu Ndg. Madadi Omari Litumbui na TALGWU itafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha haki inatendeka, aidha tunaliomba Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote waliohusika na mauaji hayo ya kinyama.

TALGWU inatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Wanachama wote kwa kuondokewa na mpendwa wetu Ndg. Madadi Omari Litumbui.

Roho ya Ndg. Madadi Omar Litumbui ipumzike kwa Amani.
Imetolewa na :
Rashid M. Mtima
KATIBU MKUU - TALGWU

No comments:

Powered by Blogger.