LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wajasiriamali Dar wanufaika na mitungi ya gesi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania, imewaahidi Mama na Baba lishe katika Soko la Samaki la Kimataifa Feri kuwafungia mtambo wa nishati safi ya kupikia ili kuwaepusha kutumia fedha nyingi kununua gesi kupitia mitungi midogo.

Imesema hatua hiyo ni utekelezaji wa mkakati wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda mazingira na kuwaweka wanawake na watoto katika nafasi nzuri ya kujiendeleza kiuchumi na kielimu.

Hayo yalielezwa jana na Mbunge wa Ilala ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge Hassan Zungu katika hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi 200 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa mama na baba lishe wa sokoni hapo Machi 22, 2024.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbasi Mtemvu, Mkuu wa Wilaya Ilala Edward Mpogolo na Mwenyekiti wa CCM wilayani humo Said Side.

Zungu alisema kuwa mitungi hiyo 200 ni sehemu ya mitungi 700 iliyotolewa kwa Mama na Baba lishe katika jimbo hilo ambayo imetolewa kwa ushirikiano wa Zungu na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania.

Naibu Spika Zungu, ametoa Oryx imetoa ahadi hiyo baada ya kupokea maombi ya wafanyabiashara hao kupitia kwa kiongozi wa wafanyabiashara wa Zone Namba 7 katika soko hilo, Said Mpinji aliyelalamika kuwa wanalazimika kutumia sh. 110,000 kila siku kujaza gesi katika mitungi inayotumika kuendeshea shughuli zao.

Akijibu kilio hicho, Zungu alisema ni ya muda mrefu na kwamba tayari amezungumza na kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu wake, Benoit Araman ambaye amekubali kufunga mifumo ya gesi ya kisasa kisha kusambaza huduma hiyo kwa wafanyabiashara hao kwa gharama nafuu.

“Mkombozi wetu ni Rais DkSamia Suluhu Hassan ambaye alianzisha kampeni ya Nishati safi ya kupikia, kuhakikisha Watanzania wanaishi maisha mazuri.

“Oryx wamekubali kuweka mtungi mmoja mkubwa na mifumo ya usambazaji, kisha watasambaza huduma kwa mama na baba lishe waliopo hapa na kuwafungia mita ambazo watzitumia kulipia huduma kama wanavyofanya katika umeme,” alisema.

Kwa upande wake Benoit alisema Oryx wamewafikia wajasiriamali hao kwa lengo la kutekeleza mkakati wa Rais Dk. Samia wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kulinda mazingira na afya za wananchi.

Alisema kuwa tangu Julai mwaka 2021, Oryx walianza mkakati huo baada ya Rais Samia kutangaza kwamba serikali yake inataka kuona hadi mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.

“Kupika kwa kutumia gesi ya Oryx kuna faida nyingi ikiwemo kuwaepusha wanawake kutumia muda mwingi kutafuta kuni, kunawaepusha watoto kwenda umbali mradi na kutumia muda wao mwingi kutafuta kuni, aida kuwasaidia kupata muda mwingi wa kujisomea,” amesema.

Mwenykiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Abbasi Mtemvu aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, amesema kilichofanyika ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kumpongeza Zungu kwa namna anavyowatetea wananchi katika jimbo lake.

“Zungu ni mfano wa kuigwa, amefanya makubwa. Nilikuwa naye bungeni kwa miaka 10 muda wote ameonyesha dhamira ya kutetea wananchi wa jimbo lake, anastahili pongezi,” almeeleza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mgolo, amesema maelekezo yaliyotolewa na Naibu Spika Zungu kutaka ifanyike tathmini haraka kufanikisha Oryx kufunga mtambo huo atayatekeleza kwa haraka kwa kushirikiana na wenzake.

Hata hivyo, aliiomba Oryx kuangalia uwezekano wa mtambo kama huo kufungwa pia katika eneo la Zone Namba 4 ambako baba na mama lishe nao wanahitaji huduma hiyo.
.Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu ( kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Meneja Mauzo wa Kampuni ya Gasi ya Orxy , Shaban Fundi (wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi ya kupikia ya Oryx Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Zone no.7 wa Soko la Samaki la Kimataifa Feri Jijini Dar es Salaam, Saidi Mpinji wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kulia).
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Happy Kiondo wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mmoja wa mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ( wa pili kulia),Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo ( wa kwanza kulia), Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle ( wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman ( wa pili kushoto) wakimkabidhi mtungi wa gesi mama lishe na mfanyabiashara katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Salma Mohammed wakati wa makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa mama lishe na baba lishe wa soko hilo leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akiwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Gesi ya Orxy, Benoite Araman wakiwasikiliza wafanyabiashara wa samaki katika soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Jijini Dar es Salaam, Mussa Zungu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam leo Machi 22, 2024.




Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi wa Kampuni ya Gasi ya Orxy, Benoite Araman akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam




Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughle akizungumza katika hafla ya kukabidhi mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri wakiwa kwenye hafla ya makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali hao, Jijini Dar es Salaam 
Meneja Masoko wa Kampuni ya Gesi ya Orxy Peter Ndomba akitoa elimu ya matumizi sahihi ya mtungi wa kupikia wa gesi ya Orxy katika hafla ya makabidhiano ya mitungi ya kupikia ya gesi ya Orxy 700 kwa wajasiriamali wa soko la Samaki la Kimataifa Feri, Jijini Dar es Salaam.
Na Emmanuel Mbatilo, Dar

No comments:

Powered by Blogger.