LIVE STREAM ADS

Header Ads

GCLA yaonya matumizi holela ya bidhaa za kemikali

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Msimamizi wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu (GCLA), Yohana Goshashy (kulia) akizungumza wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza. Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Peter Juma.
***


Wananchi wametakiwa kuzingatia matumizi sahihi ya bidhaa mbalimbali ikiwemo za viwandani ambazo hutengenezwa kwa kutumia kemikali, hatua itakayowakinga na madhara ya kiafya.

Msimamizi wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu (GCLA), Yohana Goshashy amesema matumizi ya bidhaa za viwandani kama vileo na dawa tiba yanaweza kugeuka sumu katika mwili wa binadamu ikiwa matumizi sahihi hayatazingatiwa.

"Kumekuwa na ongezeko la matukio ya wananchi kudhurika na sumu kupitia vyakula, pombe, sigara, dawa tiba na dawa za kulevya. Matukio hayo yanaacha simanzi katika familia na kupoteza nguvu kazi ya Taifa. Mwaka 2022 zaidi ya watu elfu 90 walidhurika na matukio ya sumu na mwaka 2023 kulikuwa na matukio zaidi ya laki moja. Ni jukumu letu kuelimisha jamii kujilinda na matukio ya kudhurika na sumu" amesema Goshashy.

Katika kuisaidia jamii, GCLA imetoa mafunzo ya kudhubiti matukio ya sumu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza ili kuwajengea uwezo wa kwenda kuelimisha wananchi kuchukua hatua na kujilinda na matukio ya sumu za aina mbalimbali ikiwemo zitokanazo na matumizi ya bidhaa mbalimbali hususani zinazotengenezwa kwa kemikali.

"Mfano sasa hivi kuna ongezeko kubwa la matumizi yasiyo sahihi ya vinywaji wa kusisimua mwili (energy drink). Watengenezaji wameandika kabisa, usinywe zaidi ya chupa moja kwa siku, lakini watumiaji hawazingatia tahadhari hiyo. Bidhaa za pombe zimeandikwa, unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya, lakini watumiaji hawazingatii na matokeo yake ni vinywaji hivyo kugeuka sumu mwilini na kuleta madhara ikiwemo magonjwa ya kansa" ametahadharisha Goshashy.

Goshashy amesema kutokana na suala la maendeleo, matumizi ya kemikali za viwandani hayawezi kuepukika hivyo jambo la kuzingatia ni watumiaji wa bidhaa mbalimbali kuzingatia maelezo yaliyo kwenye vifungashio vya bidhaa hizo akisema "tunaweza kuwa salama kama mara zote tutazingatia matumizi salama ya bidhaa za viwandani na kuacha kufanya mambo kwa mazoea, madhara haya yanaepukika".

"Tumekuwa tukikosea matumizi ya dawa na vileo bila kuzingatia matumizi. Mafunzo yatatusaidia kuzingatia utaratibu wa matumizi ya bidhaa zinazotokana na kemikali na tunaenda kuelimisha pia wananchi namna ya kutumia bidhaa zitokanazo na kemikali ili kuepuka madhara" amesema Mwenyekiti wa Mtaa wa Temeke jijini Mwanza, Pamela Chacha baada ya kupata mafunzo ya GCLA.

Mmoja watoa huduma za afya ngazi ya jamii jijini Mwanza, Alfred Isack amekirinkiwa wananchi hawana uelewa wa kutosha kuhusu matumizi ya kemikali hivyo kupitia mafunzo yanayotokewa na GCLA yatamsaidia kuwaelimisha kupitia mikutano ya hadhara na kuwahiniza kufuata miongozo kwa mujibu wa taratibu za utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na kemikali ikiwemo pombe na dawa tiba.

Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Peter Juma amesema matumizi yasiyo sahihi ya bidhaa za kemikali ikiwemo sabuni yamekuwa yakisababisha madhara kwa jamii.

"Jamii iepuke matumizi holela ya bidhaa zinazotengenezwa kwa kemikali ikiwemo sabuni za usafi ambazo siku hizi watu wanajitengenezea tu majumbani. Pia wazingatia kufuatilia tarehe ya ukomo wa bidhaa hizo (expire date)" amesema Juma.

Kundi la wanaume linatajwa kuwa katika hatari zaidi ya kupata madhara ya sumu mwilini kwa zaidi ya asilimia 60 ikilinganishwa na wanawake kutokana na matumizi holela na ya kupita kiasi ya bidhaa mbalimbali ikiwemo vileo, 'energe drinks' na nyinginezo na hivyo kuhimizwa kubadili mtindo wa maisha ili kuepuka madhara zaidi ikiwemo viungo vya mwili kama Figo, ini na mapafu kushindwa kufanya kazi/ ama kupata kansa.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Msimamizi wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu (GCLA), Yohana Goshashy (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Peter Juma akizungumza wakati wa zoezi la kuhitimisha mafunzo ya kudhibiti matukio ya sumu yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Mitaa jijini Mwanza.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Peter Juma akizungumza wakati wa zoezi la kuhitimisha mafunzo ya kudhibiti matukio ya sumu yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Mitaa jijini Mwanza.
Wanahabari (kushoto) wakinasa matukio wakati Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Peter Juma akihitimisha mafunzo ya kudhibiti matukio ya sumu yaliyotolewa kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Mitaa jijini Mwanza.
Mafunzo hayo yamejumuisha jumla ya washiriki 109 ambao ni pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Mitaa kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mafunzo hayo yamejumuisha jumla ya washiriki 109 ambao ni pamoja na wahudumu wa afya ngazi ya jamii, maafisa mazingira Kata na Wenyeviti wa Mitaa kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Msimamizi wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu (GCLA), Yohana Goshashy (kulia) akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Peter Juma alipowasili kuhitimisha mafunzo hayo. Kushoto ni mwakilishi wa washiriki wa mafunzo hayo.
Mwakilishi wa washiriki wa mafunzo (kushoto) akitoa shukurani na kueleza umuhimu wa mafunzo hayo.
Msimamizi wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Matukio ya Sumu (GCLA), Yohana Goshashy (kulia) akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pomoja na mgeni rasmi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.