LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana awasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi amesema kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo jijini Mwanza inaendelea kusimamiwa vizuri na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Makilagi aliyasema hayo Jumamosi Aprili 20, 2024 wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Machi 2024 katika mkutano wa Halmashauri Kuu chama hicho.

Alisema utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya kimkakati kama vile meli mpya ya MV. Mwanza, Soko Kuu, SGR na bandari ya Mwanza Kaskazini inaendelea vizuri na kuwatoa hofu wananchi kwamba miradi hiyo itakamilika kama ilivyokusudiwa.

Makilagi pia alisema katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Machi 2024 Serikali imeboresha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi ikiwemo huduma za afya kwa kuongeza upatikanaji wa dawa, kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na hivyo kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasaji.

Aidha Makilagi aliahidi kushughulikia changamoto kuhamisha miundombinu ya maji, umeme na simu ili kumwezesha mkandarasi kampuni ya Zhongmei kutoka nchini China anayejenga barabara ya Buhongwa- Igoga kwa kiwango cha lami kukamilisha kwa wakati mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 22.

Awali Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Peter Begga alieleza kutoridhwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo uliosainiwa Septemba 2023 ambapo hadi sasa uko asilimia nne badala ya asilimia saba kwa mjibu wa mkataba.

Mkandarasi amesema changamoto ni gharama kubwa zilizowasilishwa na MWAUWASA na TANESCO za kuhamisha miundombinu ya maji na umeme ambapo MWAUWASA iliwasilisha shilingi milioni 800 na TANESCO zaidi ya shilingi bilioni moja wakati fedha zilizotengwa kuhamisha miundombinu ya maji, umeme na mawasiliano ni shilingi milioni 250, nikuombe ukashughulikie suala hilo ili mradi ukamilike kwa wakati" alisema Begga.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi akizungumza wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu wa CCM wilayani humo.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Peter Begga akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu wa chama hicho wilayani humo uliolenga kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi kwa kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi Machi 2024.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Peter Begga akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu wa chama hicho.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana wakifuatilia mkutano wa uwasilishaji taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024.
Katibu wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Godfrey Kavenga (katikati) akitoa mwongozo katika mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana wakifuatiolia taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi.
Watendaji mbalimbali jijini Mwanza wakiwa kwenye mkutano huo.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.