LIVE STREAM ADS

Header Ads

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu aongoza mkutano wa TNCM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi ambaye ni Mwenyekiti wa TNCM ameongoza Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026.

Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Jengo la Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2024 na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalaum, Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Medical Stores Department (MSD), Local Fund Agent (LFA), Sekretarieti ya TNCM, Asasi za Kiraia (Non State Actors - NSAs) na Wadau wa Maendeleo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiongoza Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026. Mkutano ulifanyika ukumbi wa Jengo la Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2024.Kushoto ni Mwenyekiti wa TNCM, Kent Pius na wa kwanza kulia ni Makamu Mwenyekiti wa TNCM, Godlisten Moshi.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mtendaji wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM), Kent Pius wakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM),ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) wakifuatilia mkutano huo ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026. Mkutano ulifanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Mwenyekiti wa TNCM, Kent Pius wakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026. Mkutano ulifanyika ukumbi wa Jengo la Tume ya Ushindani Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Aprili, 2024.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Afisa Mratibu Uzingatiaji na Taratibu katika Utekelezaji wa Miradi ya Mfuko wa Dunia unaolenga Kupambana na UKIMWI, KIFUA KIKUU, MALARIA na Uboreshaji wa Mifumo na Miundombinu ya Afya (RSSH) Tanzania, Denis Eliasaph wakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Meneja Mpango wa NASHCOP, Ambwene Mwakalobo akiwasilisha kuhusu Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI, Magonjwa ya ngoni na Homa ya Ininwakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM).
Mkuu wa Dawati la Uimarishaji wa Mifumo ya Kutolea Huduma za Afya kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Hussein Athumani akiwasilisha wasilisho la Resilient and Sustainable Systems for Health (RSSH) wakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM).
Mwenyekiti wa TNCM, Kent Pius akizyngumza wakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026.
Mkuu wa Program Wizara ya Afya, Dkt. Catherine Joachime, akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Tanzania National Coordinating Mechanism (TNCM) ulilenga kujadili mikakakati mbalimbali itakayoongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa Programu za Malaria, UKIMWI na Kifua Kikuu zinazofadhiliwa na Mfuko wa Dunia katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2024 hadi 2026.
Na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments:

Powered by Blogger.