LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya TMFD yamtunuku tuzo Dkt. Biteko

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha waandishi wa habari wa kuendeleza shughuli za bahari na uvuvi Tanzania (TMFD) kimemtunuku tuzo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kutokana na jitihada zake za kusimamia na kuendeleza mradi wa umeme wa bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza wakati wa utoaji tuzo hiyo, Mkurugenzi wa chama hicho, Edwin soko amesema mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere ni alama ya kuchangamkia fursa za uchumi wa buluu hivyo wametambua jitihada za Dkt. Biteko kwenye kusimamia mradi huo.

"Dkt. Biteko anastahili tuzo hii kwa sababu tumekuwa tukimfuatilia anavyopambana kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili kumaliza changamoto ya umeme nchini na pia kufikia lengo la Serikali la kuuza umeme nchi jirani" alisema Soko.

Tuzo hiyo ilitolewa kwenye hafla ya maonesho ya picha za uchumi wa buluu iliyoambatana na kongamano la uchumi wa buluu iliyofanyika Aprili 08, 2024 ukumbi wa Mwanza Hotel jijini Mwanza. 

Zaidi ya washiriki 100 walihudhuria hafla hiyo na kupata elimu kuhusu dhana ya uchumi wa buluu na fursa zaitokanazo na vyanzo vya maji kutoka kwa wataalamu wa uchumi wa buluu.

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo alikuwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda ambaye alitoa pongezi kwa taasisi ya TMFD kwa kutambua fursa za uchumi wa buluu na kuamua kukufanyia kazi eneo hilo ambalo Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imelitengea zaidi ya shilingi bilioni 60 ili kuhakikisha linaleta tija kwa wananchi.
Mkurugenzi wa taasisi ya TMFD, Edwin Soko (kushoto) akikabidhi tuzo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (hayuko pichani) kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kulia) ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uchumi wa buluu jijini Mwanza. 
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda (kulia) akipokea tuzo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (hayuko pichani) iliyotolewa na taasisi ya TMFD. Kushoto ni Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Edwin Soko. 
Mkurugenzi wa taasisi ya TMFD, Edwin Soko akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Said Mtanda akizungumza wakati wa hafla ya maonesho na kongamano la uchumi wa buluu iliyoandaliwa na taasisi ya TMFD. 

No comments:

Powered by Blogger.