LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zaidi ya Milioni 800 zakamilisha madarasa shule ya kimataifa Isamilo, jamii yapewa ujumbe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jamii imetakiwa kujiepusha na tabia za ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto ikiwemo kuwaozesha ndoa za mapema zinazowanyima haki ya msingi ya kupata elimu na kuathiri mstakabali wa maisha yao ya baadae.

Rai hiyo imetolewa jijini Mwanza Alhamisi Aprili 25, 2024 na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN), Zephania Ntuza wakati wa hafla ya ufunguzi wa majengo mapya ya shule ya awali ya kimataifa Isamilo.

Askofu Ntunza alisema ndoa za utotoni zinawaathiri watoto kisaikolojia pamoja na kuwakatili kihisia kwani umri wao wa kuolewa ama kuoa bado unakuwa haujafika na hivyo wanashindwa lkumudu masuala ya ndoa.

"Wazazi na walezi wote pelekeni watoto shule ili waweze kupata haki yao ya elimu, mnapowaozesha katika umri mdogo mnawakosea, kanisa la Anglikana linaungana na Serikali yetu kupinga ukatili kwa watoto, ndoa za utotoni na ukeketaji kwa watoto wa kike" alisema Askofu Ntuza.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, Mchungaji Jacob Mutashi alisema wazazi wanapaswa kuwekeza kwenye elimu kwa kuwapeleka watoto shule kwani kwa kufanya hivyo ni kujiwekea akiba itakayowasaidia hapo baadae.

"Wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwaozesha watoto wao kwa tamaa ya kujipatia mali jambo ambalo linawatesa wanapozeeka kutokana na kushindwa kujikimu na kukosa msaada" alisema Mchungaji Mutashi wa kanisa la EAGT Kiloleni wilayani Ilemela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kojas Builders iliyotekeleza ujenzi huo, Nyerere Lucas alisema mradi huo umegharimu shilingi milioni 800 ukihusisha majengo saba yakiwemo manne yenye madarasa mawili, jengo la utawala, maktaba na jengo la watumishi.

Awali Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela, Mariam Msengi alisema Serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki ya watoto kusoma ikiwa ni pamoja na kujenga shule mpya za msingi na sekondari, elimu bila malipo pamoja na kuboresha miundombinu ya kujifunzia.
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela, Mariam Msengi (kushoto) na Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Victoria Nyanza (DVN, Zephania Ntuza (kulia) wakikata upete kuashiria ufunguzi wa majengo mapya ya madarasa katika shule ya kimataifa Isamilo jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Ilemela, Mariam Msengi akizungumza kwenye hafla fupi ya ufunguzi wa majengo mapya ya shule ya awali ya kimataifa ya Isamilo jijini Mwanza.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya kimataifa ya Isamilo jijini Mwanza wakitoa burudani kwenye hafla ya ufunguzi wa majengo mapya ya shule ya awali ya kimataifa ya Isamilo iliyopo jijini Mwanza.
PIA SOMA>>> Habari zaidi hapa

No comments:

Powered by Blogger.