LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanahabari watembelea vizimba vya samaki, kuelekea kongamano la TMFD

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waandishi wa habari jijini Mwanza kupitia taasisi ya waandishi habari wa kuendeleza shughuli za bahari na uvuvi Tanzania (TMFD) wametembelea visimba vya ufugaji samaki katika Ziwa Victoria ili kujifunza kuhusu uendeshaji wa shughuli hiyo kwa ajili ya kuelimisha jamii ya wafugaji.

Ziara ya kutembelea vizimba hivyo imefanyika Jumatatu Aprili 08, 2024 kuelekea maonesho na kongamano la uchumi wa buluu yaliyoandaliwa na TMFD katika ukumbi wa Mwanza Hotel.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Elpidius Mpanju ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya My fish Tanzania inayofuga samaki kwa njia ya vizimba eneo la Luchelele jijini Mwanza, amesema ufugaji samaki una tija zaidi tofauti na uvuvi wa asili ambao mvuvi hana ukakika wa kupata samaki wa kutosha.

Mpanju amesema ufugaji samaki kwa njia ya vizimba unakwenda kutatua changamoto ya uhaba wa samaki katika Ziwa Victoria ambao umesababishwa na mahitaji ya samaki kuongezeka huku mazalia yakipingua kutokana na changamoto za uhabaribu wa mazingira.

Naye Darius Salvatory ambaye ni Msimamizi wa fukwe ya 'Stress Free' inayoendeshwa na jeshi la magereza katika eneo la Butimba jijini Mwanza amesema ufugaji samaki katika fukwe hiyo umeongezwa chachu kwa wateja ambapo hupata fursa ya kufanya utalii wa uvuvi kwa kuvua samaki kwa ajili ya kitoweo.

Kwa upande wake Mratibu wa TMFD, Betty Massanja amesema kongamano na maonesho ya uchumi wa buluu limelenga kuongeza uelewa kwa waandishi wa habari kufahahamu na kuchangamkia fursa za uchumi wa buluu.

Amesema waandishi wa habari wakizifahamu fursa za uchumi wa buluu ambazo ni pamoja na ufugaji samaki njia ya vizimba, watashiriki kwenye shughuli hizo na kujiongezea kipato huku pia wakiendelea kuelimisha wananchi kupitia vyombo vya habari.

"Tumebaini bado kuna fursa kwenye uchumi wa buluu kupitia vyanzo tulivyonavyo, tuna Ziwa Victoria pamoja na bahari ya Hindi, tusibaki nyuma kuchangamkia fursa hizo" amesema Esther Baraka, mwanahabari wa Afya Radio.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Elpidius Mpanju ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya My fish Tanzania akitoa ufafanuzi wa kwa andishi wa habari kuhusu ufugaji samaki kwa njia ya vizimba.
Elpidius Mpanju ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya My fish Tanzania akitoa ufafanuzi wa kwaandishi wa habari kuhusu ufugaji samaki kwa njia ya vizimba.
Darius Salvatory ambaye ni Msimamizi wa fukwe ya 'Stress Free' inayoendeshwa na jeshi la magereza katika eneo la Butimba jijini Mwanza akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari waliotembelea ufukwe huo kujifunza kuhusu utalii wa uvuvi ndani ya Ziwa Victoria.
Mratibu wa TMFD, Betty Massanja (kulia) akimsikiliza Thomas Philp ambaye ni mwongoza watalii katika ufukwe wa Stress Free jijini Mwanza.
Waandishi wa habari jijini Mwanza wakiwa kwenye ufukwe wa Stress Free.
Wanahabari wakiwa 'Stress Free Beach" jijini Mwanza kabla ya kuelekea kwenye maonesho na kongamano la uchumi wa buluu yaliyoandaliwa na TMFD katika ukumbi wa Mwanza Hotel, Jumatatu Aprili 08, 2024.
Wanahabari wakiwa Ziwa Victoria kujifunza kuhusu fursa za uchumi wa buluu.
Wanahabari Mwanza wakijifunza kuhusu utalii wa uvuvi katika fukwe ya Stress Free.
Mratibu wa TMFD, Betty Massanja akifanya mahojiano kuhusu fursa za uchumi wa buluu ambazo zinajumuisha rasilimali zinazopatikana kwenye maji.

No comments:

Powered by Blogger.