LIVE STREAM ADS

Header Ads

Michuano ya 'Chuo Challange Cup 2024' kutimua vumbi Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Michuano ya soka ya ‘Chuo Challenge Cup 2024’ inarajia kuanza kutimua katika dimba la Nyamagana jijini Mwanza, ikishirikisha vyuo vya kati na vyuo vikuu 16 ikiwa inafanyika kwa msimu wa tatu mfululizo mwaka huu.

Mratibu wa michuano hiyo, Dickson Mpilipili ambaye pia ni mtangazaji wa michezo Sahara Media amesema pazia la michuano hiyo linatarajiwa kufunguliwa Aprili 20, 2024.

Timu zote shiriki tayari zimekabidhiwa jezi katika hafla iliyofanyika Aprili Ijumaa Aprili 05, 2024 ambapo jezi hizo zimetolewa na mmoja wa wadhamini ambaye ni mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.