LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bingwa wa masoko, Chris Diaz ateuliwa kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa 'ADIL Group'

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya 'ADILI Group' na kampuni zake tanzu za ALN Kenya na ALN Tanzania imteua mtaalamu wa masoko duniani, Chris Diaz kuwa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi wa Ukuaji na Masoko Mapya wa kampuni hiyo.

Diaz ametoa matokeo makubwa ya kibiashara na kuongoza mageuzi makubwa kwa mashirika aliyoongoza ikiwa ni pamoja na Bidco Africa alikohudumu kwa miaka 16.

Uteuzi wa Chris ni wa kimkakati na wakuimarisha utoaji wa huduma zilizounganishwa na mteja kwa njia mbalimbali za kibiashara ambapo hatua hiyo inalenga kukuza ushirikiano na kuendeleza teknolojia ya kisasa.

Kampuni ya Adili Group na kampuni zake tanzu imekuwa bora zaidi katika nafasi ya kukabiliana kwa haraka na mazingira yanayoendelea ya huduma za ushauri wa kisheria na kimkakati.

Aidha Chris atatumia uzoefu wake kuwapa wateja maarifa na suluhisho linalohitajika ili kukabiliana na changamoto za kampuni ikiwa ni pamoja na kusimamia usumbufu wa biashara na kuongoza mwelekeo wa kimkakati kwa kupanua wigo wa masoko yaliyopo na mapya huku akiimarisha hadhi ya kampuni za Adili.

No comments:

Powered by Blogger.