LIVE STREAM ADS

Header Ads

Duka jipya la vipodozi lafunguliwa Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mfanyabiashara Maarufu mjini Shinyanga Georgia Buyamba amezindua duka la kipekee la vipodozi na manukato ‘Unique Skin & Scents’ likiwa limesheheni bidhaa mbalimbali za urembo wa ngozi na manukato kwa ajili ya wanawake, wanaume na watoto.

Duka la Unique Skin & Scents lililopo Mjini Shinyanga mkabala na Benki ya CRDB Shinyanga limezinduliwa rasmi Ijumaa Mei 17,2024.

Mkurugenzi wa Unique Skin & Scents, Georgia Buyamba amewakaribisha wakazi wa Shinyanga na maeneo jirani kufika katika duka hilo kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya bidhaa za urembo wa ngozi na vipodozi vyenye ubora wa hali ya juu na kwa bei rahisi kabisa.

"Ninapenda kuwakaribisha sana wateja wetu, Njooni Unique Skin & Scents mjipatie bidhaa za urembo wa ngozi na manukato mazuri,. Tuna vitu vingi vizuri, vya kipekee, vyenye ubora, Original, kwa kweli tuna vipodozi na manukano ya kila aina kwa ajili ya wanaume, wanawake na watoto kutoka Dubai, UK, USA " amesema Buyamba.
Mfanyabiashara Maarufu mjini Shinyanga Georgia Buyamba akielezea kuhusu bidhaa zinazopatikana katika Duka la kipekee la Vipodozi na Manukato ‘Unique Skin & Scents’ lililopo Mjini Shinyanga Mkabala na Benki ya CRDB Shinyanga.
Mfanyabiashara Maarufu mjini Shinyanga Georgia Buyamba akionesha bidhaa zinazopatikana katika Duka la kipekee la Vipodozi na Manukato ‘Unique Skin & Scents’ lililopo Mjini Shinyanga Mkabala na Benki ya CRDB Shinyanga.

No comments:

Powered by Blogger.