LIVE STREAM ADS

Header Ads

Barabara ya Dar-Lindi-Mtwara sasa Shwari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Barabara ya Dar es salam-Lindi-Mtwara sasa imerejea katika hali ya kupitika baada ya kukamilika urejeshaji wa mawasiliano katika maeneo yote yaliyokuwa yamekatika.

Mvua kubwa zilizoambata na kimbunga Hidaya ziliharibu miundombinu ya barabara hiyo katika eneo la Mikereng’ende, Songas, Somanga na Matandu-Nangurukuru ambayo yalikatika kutokana na mvua zilizonyesha na kuambatana na Kimbunga Hidaya.

Juzi tarehe 09 Mei 2024 magari ya mizigo, mabasi na magari mengine madogo yaliyokwama yalianza kuruhusiwa kuendelea na safari jambo ambalo liliamsha hisisa mseto kwa wananchi kuwapongeza wataalamu wa Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala ya Barabara (TANROADS) kwa kazi waliyoifanya usiku na mchana katika kurejesha miundombinu hiyo.

Wakati huu wa mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali, wananchi, wasafiri, wasafirishaji na watumiaji wengine wa barabara wanapaswa kusafiri kwa tahadhari kwani maeneo mengine yanaendelea na matengenezo.

No comments:

Powered by Blogger.