LIVE STREAM ADS

Header Ads

Fahamu zaidi kuhusu haki ya mtandao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kama zilivyo haki za makundi mengine mfano, haki za binadamu, haki ya uhuru wa kujieleza na kusikilizwa. Haki ya kupata taarifa kwa wakati sahihi, ndivyo zilivyo Haki za mtandao (digital rights) na kanuni zake ambazo ni msingi kwa uongozi bora wa mtandao wa internet. Kanuni zimekusanywa kwa muungano wa haki na kanuni za mtandao (Dynamic Coliation on Internet Rights and Principples).

Mtandao umetoa fursa nyingi za kipekee kwa ulimwengu, Kwa utambuzi wa haki za kibinadamu na kuepuka unyanyasaj. Hali kadhalika jukumu la matumizi ya mtandao katika maisha yetu ya kila siku linazidi kuongezeka.

Hivyo ni muhimu kwa serikali, mashirika ya umma na taasis za kibinafsi, watu binafsi kuheshimu na kulinda haki za kibinadamu kwenye mtandao.

Miaka ya nyuma kabla ya kukua kwa sekta ya mtandao/ tovuti, mambo mengi yalikua ni magumu kueleweka ama kufanyika katika jamii pia asilimia karibu 60% haikua na uelewa juu ya matumizi sahihi ya mtandao, lakini kupitia tovuti jamii kubwa wamepata fursa ya kujua haki zao za msingi. Jamii inafanya biashara kubwa mtandaoni na kuongeza pato la Taifa.

Mawasiliano yamerahisishwa baina ya Taifa kwa Taifa, mtu kwa mtu. Kupitia haki za kimtandao baadhi ya mataifa wamepata kujifunza juu ya demokrasia kutoka mataifa kadhaa kujifunza kutoka kwa Taifa jingine kwa habari sayansi ya siasa na maendeleo.pia Taifa lao liko katika hatua gani katika siasa, uchumi, afya pamoja na ulinzi na usalama.

Pamoja na haki hizo muhimu za kimtandao, bado kuna changamoto nyingi kwani huduma ya mtandao haipatikani kwa usawa au haiwafikii watu wote na hivyo inakuza ukosefu mpya wa usawa kulingana na jinsia, jografia, kipato na ujuzi wa kidijatli na kuongeza udhaifu kwa wale waliotengwa zaidi katika jamii.

Takwimu zinaonyesha katika mwaka 2019 mtandao ulizimwa mara 200 kwa nchi 33 ikiongozwa na nchi ya India, kwa takwimu hizi visa vingi vya kufungwa kwa mtandao ndani ya mwaka 2019 vilifanyika Bara la Asia.

India ikiongoza, mtandao wa simu za mkononi ulizimwa mara 21 inchini humo ambapo ni sawa na asilimia 67%. Hapa kwetu Tanzania kumekuwa na matumio kadhaa hasa katika kipindi cha uchaguzi 2020 mtandao ulishuka na maeneo mengine kutopatikana kabisa, hivyo wafanyabiashara wa mtandaoni na makundi mbali mbali ya watumiaji wa mtandao walikumbana na hasara na hata mapato kushishuka kutokanana kadhia za kimtandao.

Kupitia changamoto hizo, taasisi ya 'Zaina Foundation' inayojihusisha kuhamasisha wanawake na watoto (makundi yaliyosabaulika), matumizi sahii na salama ya mtandao, huku likiamini kuwamatumizi ya ya Internet ni haki ya msingi ya binadamu. 

Hivyo shirika hilo limekuja na kampeni yake ya #KeepItOn. Kampeni hii ni mahususi Kwa wenye mamlaka na watoa huduma ya mtandao kuwakumbusha kutokuzima mtandao ama kupunguza kasi yake.
Imeandaliwa na Deborah Mallaba, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.