Redio Afya yapeleka furaha kwa zaidi ya wanafunzi 700 Mwanza
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Redio Afya 96.9 Mwanza imepeleka furaha kwa zaidi ya wanafunzi wa kike 700 wa shule ya sekondari Buzuruga wilayani Ilemela, baada ya kuwakabidhi taulo za kike kupitia kampeni yake ya Furaha ya Binti ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Hedhi Salama Duniani yaliyofanyika Mei 28, 2024. *** |
Imeelezwa kuwa baadhi ya familia haziwezi kumudu gharama za kununua taulo za kike, hali inayochangia wanafunzi wa kike kukosa masomo wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Hayo yalielezwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Buzuruga iliyopo Manispaa ya Ilemela, Betha Daniel katika zoezi la kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule hiyo kupitia kampeni ya Furaha ya Binti.
Kupitia kampeni iliyoratibiwa na 96.9 Redio Afya Mwanza, Mwl. Betha alisema wameipokea vizuri na kwamba taulo za kike zilizo tolewa shuleni hapo zitawasaidia wanafunzi wa kike kujistiri wakati wa hedhi.
“Mimi nimefurahishwa na hii kampeni kwa sababu imewahamasisha wanafunzi wameweza kujitambua kama ambavyo mmetoa elimu kwa wanafunzi wa kiume ili pia wasiweze kuona ajabu pindi binti anapokuwa kwenye hedhi” alisema Betha.
Naye mlezi wa wauguzi kutoka katika Hospitali ya Mwananchi iliyopo jijini Mwanza, Rita Lyamba aliwataka wanafunzi wakike kuzingatia usafi wanapokuwa katika kipindi cha hedhi ili kudhibiti kupata magojwa yasiyo yalazima.
Aliwataka wanafunzi hao kutokuwa na aibu wanapokuwa kwenye hedhi na kuwashirikisha walimu wanapopata changamoto.
Baadhi ya wanafunzi waliopata elimu hiyo walishukuru kupatiwa elimu hiyo kwakuwa imeongeza uelewa wao ambapo wanafunzi wakiume wameahidi kuwasaidia wasichana wanapopata changamoto ya hedhi.
Zoezi hilo limeratibiwa na 96.9 Afya Radio Mwanza kupitia kampeni yake ya Furaha ya Binti ambapo wadau mbalimbali wamefanikisha upatikanaji wa taulo za kike na kukabidhiwa kwa zaidi ya wanafunzi wa kike 700 wakati wa maadhimisho ya siku ya hedhi salama duniani yaliyofanyika Mei 28, 2024.
Wadau waliofanikisha kampeni hiyo ni pamoja na UWURA, UTPC, TIRA, NIC, Jubilee Insurance, ONA Eye Care, Paradise at Home na African Child Comforters Organization.
Meneja wa redio Afya, Idd Juma akizungumza wakati wa kutoa elimu na kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buzuruga.
Meneka wa Vipindi redio Afya, Madam Esther Baraka ambaye pia aliratibu kampeni ya kutoa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buzuruga akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule hiyo.
Msimamizi wa wanafunzi wa kike shule ya sekondari Buzuruga (Matroni), Mwl. Esther Venance (kulia) akihojiwa na mwanahabari kutoka redio Afya.
Mtangazaji wa redio Afya akizungumza wakati wa kampeni ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buzuruga.
Mmoja wa wanafunzi akiuliza swali kuhusu hedhi salama.
Mwanafunzi shule ya sekondari Buzuruga akiuliza swali.
Zoezi la utoaji elimu kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buzuruga kuhusu hedhi salama.
Wanafunzi wakielimishwa kuhusu hedhi salama.
Wanafunzi wakipewa elimu kuhusu hedhi salama na namna ya kutumia taulo za kike.
Baadhi ya watumishi wa redio Afya wakiwa kwenye kampeni ya kukabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Buzuruga.
Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Buzuruga wakikabidhiwa taulo za kike kupitia kampeni ya Furaha ya Binti.
Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Buzuruga wakifurahia baada ya kukabidhiwa taulo za kike kupitia kampeni ya Furaha ya Binti iliyoratibiwa na redio Afya.
Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Buzuruga wakifurahia baada ya kukabidhiwa taulo za kike kupitia kampeni ya Furaha ya Binti iliyoratibiwa na redio Afya.
Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Buzuruga wakifurahia baada ya kukabidhiwa taulo za kike kupitia kampeni ya Furaha ya Binti iliyoratibiwa na redio Afya.
Wanafunzi wa kike shule ya sekondari Buzuruga, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo na wafanyakazi wa redio Afya wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wadau na wafanyakazi wa redio Afya wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mwalimu Mkuu shule ya sekondari Buzuruga.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: