LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maboresho ya mfumo wa Luku kufanyika mikoa ya Kanda ya Ziwa, Magharibi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limewahimiza wateja wake katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kushiriki zoezi la maboresho ya mfumo wa luku kuanzia Juni Mosi 2024.

Mikoa hiyo ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Tabora, Simiyu, Geita, Kagera na Katavi ambapo tayari zoezi hilo limefanyika kwa ufanisi katika Mkoa wa Kigoma.

Lengo ni kuboresho mfumo wa luku kwa kuongeza ufanisi na usalama ambapo litaendelea katika mikoa yote nchini hadi kufikia Novemba 24, 2024.

Hayo yameelezwa Alhamisi Mei 30, 2024 jijini Mwanza na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TANESCO, Irene Gowelle wakati akizungumza na wanahabari.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa shirika hilo, Irene Gowelle akizungumza na wanahabari jijini Mwanza kuhusu maboresho ya mfumo wa luku kwa wateja wa mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kuanzia Juni Mosi 2024.
Wanahabari jijini Mwanza wakifanya mahojiano na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa shirika hilo, Irene Gowelle kuhusu maboresho ya mfumo wa luku kuanzia Juni Mosi 2024 katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.