Balozi Kasike amtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji, Phaustine Kasike leo amemtembelea Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi na kufanya mazungumzo kuhusu fursa za usafiri wa anga kati ya Tanzania na Msumbiji.
Viongozi hao wamekubaliana kuangalia uwezekano wa ATCL kutumia fursa hizo ili kutanua wigo wa biashara. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Makao Makuu ya ATCL.
No comments: