LIVE STREAM ADS

Header Ads

TIRA yatoa mafunzo kwa Wanahabari, Mawakili jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imetoa mafunzo kwa waandishi wa habari na mawakili jijini Mwanza ili kuwajengea uwezo kufahamu masuala mbalimbali ya bima.

Mafunzo hayo yamefanyika Ijumaa Juni 21,2024 ikiwa ni maendelezo wa mamlaka hiyo kutoa mafunzo na elimu kwa wadau mbalimbali kuhusu umuhimu wa huduma za bima.

Meneja wa TIRA Kanda ya Ziwa, Richard Cheumbe amesema mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari na mawakili kufahamu masuala ya bima na kusaidia kuelimisha wananchi kupitia shughuli zao.

Cheumbe amesema Serikali imewekeza katika mifumo ya bima kwa ajili ya utoaji taarifa za bima hivyo ni vyema wananchi wakafuatilia na kuzingatia taarifa hizo na kuondokana na changamoto wakati wa majanga.

"Mfano kwenye magari, usikubali kupanda gari ambalo halina bima maana ikitokea ajali utapata changamoto ya fidia. Pia hakikisha unapewa tiketi maana ndio uthibitisho kwa ajili ya kupata haki" amesema Cheumbe.

Pia ameongeza kuwa huduma za bima zimeongezeka katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, vyombo vya moto, nyumba na kilimo hivyo ni vyema wananchi wakajiunga na huduma hizo ili kupata fidia wakati wa majanga.

Akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo, Mwanasheria Mwandamizi wa TIRA Kanda ya Ziwa, Wakili Aderickson Njunwa amesema waandishi wa habari na mawakili wanayo nafasi kubwa ya kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya bima ili kupata haki zao za madai, malalamiko na migogoro katika masuala ya bima.

"Tuwe mabalozi wa kuelimisha kuhusu masula ya bima ambapo MPC kwa kushirikiana na TIRA tunaweza kuanzisha tuzo za waandishi bora wa bima ili kuhamasisha zaidi undishi wa habari za bima" amesema Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Ziwa, Richard Toyota Cheumbe akizungumza kwenye mafunzo kwa kuwajengea uwezo mawakili na waandishi wa habari mkoani Mwanza kuhusu masuala ya bima.
Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Kanda ya Ziwa, Richard Toyota Cheumbe akizungumza kwenye mafunzo kwa kuwajengea uwezo mawakili na waandishi wa habari mkoani Mwanza kuhusu masuala ya bima.
Mwanasheria Mwandamizi TIRA Kanda ya Ziwa, Wakili Aderickson Njunwa akiwasilisha mada kuhusu masuala ya bima kwa mawakili na waandishi wa habari mkoani Mwanza.
Mwanasheria Mwandamizi TIRA Kanda ya Ziwa, Wakili Aderickson Njunwa akiwasilisha mada kuhusu masuala ya bima kwa mawakili na waandishi wa habari mkoani Mwanza.
Picha: Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.

No comments:

Powered by Blogger.