LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya AZZAN SPORTS yahimiza jamii kufanya mazoezi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu malumu wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwa lengo kuweka mwili sawa kiafya ili kujikinga na maradhi mbalimbali yakiwemo yasioambukiza.

Rai hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Azzan Sports Foundation, Iddi Azzan wakati wa Tamasha la Michezo liliofanyika katika uwanja wa barafu Magomeni Makuti.

"Bonanza hili malumu la kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi, tumeandaa sisi Barafu Jogging kwa kushirikiana na Chama cha Jogging Kinondoni (KIJA) pamoja na Wizara ya Afya’" amesema Azzan.

Ameishauri Jamii kufanya mazoezi kwajili ya kujikinga na maradhi yasioambukiza kwa kuwa mazoezi ni muhimu huku pia akiishukuru Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuendelea kuhamasisha jamii katika kufanya mazoezi.

"Mazoezi ni muhimu sana na tunapata sapoti kubwa sana kutoka Serikalini kupitia Wizara ya Afya na wao wamekuwa wakitusaidia sana katika hili. Kauli mbiu yetu ya ‘Mtu Ni Afya’, lazima tuendelee nayo kwa kuwa bila afya huwezi kufanya chochote" amesema Azzan na kuongeza kuwa mazoezi yatasaidia kuimarisha afya kuanzia watoto mpaka watu wazima.

Naye Mkurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli Kapologwe ameshukuru sana muitiko wa wananchi kuweza kufika katika tamasha hilo. Amesema lengo kubwa la Wizara ya Afya ni kuhamasisha ikiwa ni utekelezaji wa kampeni ya ‘Mtu Ni Afya’ ilizinduliwa na makamu wa Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Philip Mipango na kusimamiwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Amesema bado tunaendelea kufanya uhamasishaji mazoezi mazoezi pekee yake hayatoshi lazima yaendane na ulaji chakula ulio sahihi.

"Tumekuwa tukifanya uhamasishaji wa kampeni ya ‘Mtu Ni Afya’ na kampeni imejikita katika maeneo makuu matatu ambapo moja ni kupambana na magonjwa yasiokuwa ya kuambikiza kama magonjwa ya kisukari, shinikizo la damu pamoja na kansa" amesema.

Akielezea zaidi kuhusu ufanyaji mazoezi,Kapologwe amesema mazoezi yanasaidia sana kuimarisha kinga ya mwili pamoja na kusaidia katika afya ya akili.

Katika hatua nyingine, mratibu wa mradi wa ‘Mtu Ni Afya’, Anyitike Mwakitalima amesema kampeni yao inalenga Jamii yote ya watanzania inakuwa na afya bora na msingi mkubwa wa kampeni hiyo ni kinga dhidi ya maradhi.

No comments:

Powered by Blogger.