LIVE STREAM ADS

Header Ads

Maonesho ya elimu, ujuzi na ubunifu yahitimishwa jijini Tanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Maadhimisho hayo yalikuwa yamehusisha vyuo vyote vikuu na vya kati Tanzania, lengo likiwa ni kutoa nafasi kwa vyuo kuonesha ubunifu wa kutoa Elimu na ujuzi wa kufundisha wanafunzi pindi wawapo vyuoni.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho hayo, Mkuu wa Chuo cha Afya Kolandoto Shinyanga, Paschal Shiluka alisema yamekuwa kivutio kwa wana Tanga na nchi nzima kwa ujumla kwa kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi.

Alisema kama taasisi ya chuo cha Afya wamenufaika na maadhimisho hayo kwa kujitangaza kwa wananchi wa jiji la Tanga kwa njia mbalimbali, hivyo wanaamini katika mwaka wa masomo 2024/2025 watapokea wanafunzi wengi kutoka ukanda wa Tanga na viunga vyake.

Maadhimisho hayo yaliyoanza Mei 25, 2024 yakiwa na kauli mbiu isemayo "elimu, ujuzi na ubunifu kwa uchumi shindani" yamehitimishwa Mei 31, 2024 katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal jijini Tanga na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ambaye alikuwa Mgeni rasmi.
Maadhimisho ya kitaifa ya elimu, ujuzi na ubunifu yamehitimishwa Ijumaa Mei, 31 2024 jijini Tanga.

No comments:

Powered by Blogger.