Makubaliano ya miradi ya CSR yasainiwa wilayani Kishapu
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson (kulia) na Meneja Mahusiano WDL Bernard Thomas Mihayo (kushoto) Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri wakikabidhiana hati waliyotia saini makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi cha Bilioni moja itakayotekeleza jumla ya miradi 12.

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakitia saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi CSR na mgodi wa WDL kiasi cha Tsh.1,000,000,000/= itakayotekeleza jumla ya miradi mbalimbali kumi na mbili (12) kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Na Sumai Salum - Kishapu
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imesaini makubaliano (MoU) na mgodi wa Williamson Diamond Limited kwa ajili ya utekelezaji miradi 12 ya CSR yenye thamani ya shilingi bilion moja (1,000,000,000) kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Akizungumza kwenye Hafla fupi iliyofanyika Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya, Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Fatma Mohamed ameipongeza kampuni hiyo ya madini WDL na amewataka kushirikiana na wataalamu wa halmashauri watekeleze kwa wakati huku wakizingatia ubora wa miradi.
"Ndugu zangu tunajivunia kuwa na wawekezaji kama ninyi katika Wilaya yetu kwani kwa kiasi hiki cha CSR kitasaidia jamii zote zinazozunguka Mgodi huu, hivyo nendeni mkae pamoja na wataalamu huku mkizingatia kasi ya utekelezaji miradi na si hivyo tu Bali zaidi sana ni kuangalia ubora wa miradi yenyewe" amesema Fatma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson amesema hati hiyo ya makubaliano imezingatia sheria za madini sura ya 123 ya kanuni za mmiliki wa leseni za madini za mwaka 2023 na kutolewa mwongozo na TAMISEMI mwaka 2022 kwa mamlaka za serikali za mitaa kuhusu uwajibikaji kwa jamii kwa makampuni yenye leseni za madini.
Johnson amesema fedha hizo kutoka Williamson Diamonds Limited (WDL) zitasaidia kukuza kipato cha Halmashauri na jamii husika hivyo kupelekea kubadilisha maisha ya wananchi kwani watapata huduma bora na muhimu katika jamii wanazoishi.
"Kipekee tunaishukuru serikali ya Mhe. Samia Suluhu kwa kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji hata kupatikana kwa fedha na mipango ya kutekeleza miradi ya CSR kwa Halmashauri yetu hakika tutasimamia vyema fedha hizi kwa masilahi ya Halmashauri" ameongeza Mkurugenzi wa Kishapu.
Aidha Meneja Mahusiano kutoka WDL, Bernard Thomasi Mihayo ameipongeza Halmashauri hiyo na wako tayari kuhudumia jamii zinazowazunguka kwa kile wanachokipata.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu, Willium Jijimya amewapongeza WDL na kuwasihi waendelee na uzalishaji kwa wingi ili fedha hizo wanazorudisha kwa jamii ya mzunguko iongezeke zaidi.
Kwa upande wa mwakilishi wa madiwani wa mzunguko, Abdul Ngoromole amesema wakati wa utekelezwaji miradi hiyo ya maendeleo izingatie kuajiri mafundi hasa wa vijiji husika kwani itawasiaida kunyanyua vipato vya mtu mmoja mmoja na kuhudumia familia zao.
Fedha hizo za CSR zitatekeleza ujenzi wa zahanati ya Wizunza,Uanzishwaji ujenzi jengo la Mama na Mtoto kituo cha afya Maganzo,Ujenzi wa matundu Matano (5) ya vyote,Kichomea taka na ujenzi wa nyumba ya mtumishi 2 kwa 1 katika zahanati ya Mpumbula,Kuendeleza ujenzi wa jengo la OPD na RCH kituo cha afya Idukilo,Kuanza ujenzi wa uzito wa waya mita 450 shule ya sekondari Mwadui Lohumbo, ukamilishaji madarasa mawili na ofisi shule shikizi Mwamala (Wishiteleja), ujenzi wa ofisi ya Kata ya Mondo ambapo miradi hiyo saba itafanikishwa kwa 40% ya fedha hizo (400,000,000).
Ujenzi wa jengo la abiria katika stendi ya basi Maganzo, ujenzi wa maegesho ya gari za abiria stendi ya basi Maganzo, kuboresha miundombinu ya mnada wa Upili Kata ya Kishapu, ujenzi wa mradi wa umwagiliaji Kijiji cha Iyenze na ufuatiliaji na usimamizi wa miradi ya CSR 10% ambapo miradi hiyo itakamilishwa mwa 60% ya fedha hizo (600,000,000).
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakitia saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi CSR na mgodi wa WDL kiasi cha Tsh.1,000,000,000 itakayotekeleza jumla ya miradi mbalimbali kumi na mbili (12) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ,Emmanuel Johnson (suti ya kijivu) na Meneja Mahusiano WDL Bernard Thomas Mihayo (shati ya bluu) wakikabidhiana hati waliyotia saini makubaliano (MoU) ya utekelezaji Miradi ya CSR kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kiasi cha Bilioni moja itakayotekeleza jumla ya miradi 12.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga ambaye ni Katibu Tawala Wilaya hiyo na mgeni rasmi, Fatma Mohamed akizungumza kwenye tukio la utiaji saini kati ya Kishapu DC na WDL fedha za CSR Tsh.1,000,000,000 Juni 27,2024 katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambaye ni Katibu Tawala Wilaya hiyo na mgeni rasmi Fatma Mohamed akizungumza kwenye tukio la utiaji saini kati ya Kishapu DC na WDL fedha za CSR Tsh.1,000,000,000.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Emmanuel Johnson akisoma taarifa ya utiaji saini hati ya makubaliano ya utekelezaji miradi ya CSR na mmiliki wa leseni ya madini WDL.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Francis Mashenji.
Diwani wa Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Abdul Ngoromole.
Maafisa kutoka kampuni ya madini ya WDL, kushoto ni Hilda George Hizza (Afisa malalamiko WDL) katikati ni Bernard Thomas Mihayo (Meneja Mahusiano WDL) na kulia ni Sylvia Leonidas Mulongo (Mwanasheria WDL).
No comments: