RAS Mwanza awataka watumishi Ukerewe kufanya kazi kwa weledi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Akizungumza kwenye baraza la madiwani la Halmashauri hiyo liliyokutana kujadili hoja za CAG za Juni 2023, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya alibainisha kuwa kumekuwa na kasumba ya kutompa ushirikano mzuri CAG na matokeo yake hoja kuchukua muda mrefu kumalizwa.
"Nawapongeza kwa kuwa na hati safi kwa miaka mitatu mfululizo, lakini ongezeni bidii katika mapato ya ndani ili muwe na miradi yenye tija kwa wananchi" alisema Balandya.
Aidha aliwataka madiwani kudhibiti na kusimamia vizuri miradi ya maendeleo ambayo itachangia kuongeza kipato na hali bora kwa wananchi
"Halmashauri ya Ukerewe katika hesabu za mwaka 2023 ilikuwa na hoja 3,018 ambapo zimemalizwa hoja nane zipo hatua ya utekelezaji na 4 zimejirudia" alisema John Mashimo kutoka ofisini ya CAG.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Christopher Ngubiagai akitoa hotuba ya shukran aliomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuongeza idadi ya watumishi ili kuongeza ufanisi wa kazi.
"Ndugu Katibu Tawala hapa Halmashauri tuna upungufu wa watumishi kwa 53%, yupo Mwanasheria mmoja tu hivyo akipata dharura mambo mengi yanakwama" Mkuu wa Wilaya.
No comments: