Timu ya soka ya TPDC yaendelea kujinoa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Mapema asubuhi ya Julai 21, 2024 timu ya mpira wa miguu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imecheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Tanga All stars katika uwanja wa Mikocheni TPDC.
Mchezo huo uliokuwa wa kasi na wakuvutia kwa pande zote mbili umemalizika kwa TPDC kuvuna point tatu kwa ushindi wa bao 5-3.
Waliocheka na nyavu ni mshambualiaji Donald Aponde (43), Ismail Naleja (55), Dalushi Shija (65), Isack Mtei (75) na George Leonard (89).
Ikumbukwe kuwa michezo hii ya kirafiki ni sehemu ya mazoezi kwa timu ya TPDC kuelekea mashindano ya SHIMMUTA yatakayofanyika Novemba, 2024 jijini Tanga.
Kocha wa timu ya TPDC, Bizoo Bituka amesema kuwa ameridhishwa na maandalizi ya kikosi na kikosi kipo tayari kwenda kupeperusha vyema bendera ya TPDC katika mashindano ya SHIMMUTA.
''Mpaka sasa maendeleo ya timu ya TPDC ni mazuri kwani hadi sasa tumecheza michezo ya kirafiki mitano (5) na hatujapoteza mchezo wowote'' aliongea kocha Bizoo.
1.TPDC 4 VS 1MRC
2.TPDC 3 VS 1 DIT
3.TPDC 3 VS 1Mkemia Mkuu
4.TPDC 5 VS 1 Umoja Veteran
5.TPDC 5 VS 3 Tanga All stars
No comments: