LIVE STREAM ADS

Header Ads

CRDB Kanda ya Ziwa wazindua kampeni ya 'SimBanking Transact By Finger' awamu ya pili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa imezindua awamu ya pili ya kampeni ya 'SimBanking Transact By Finger, Road To Desember', kwa lengo la kuhamasisha wafanyakazi wake kuongeza juhudi katika kuwahudumia wateja.

Akizindua kampeni hiyo Jumamosi Julai 06, 2024 katika tawi la CRDB Nyerere jijini Mwanza, Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta amesema kupitia kampeni hiyo, wateja wataelimishwa kupata huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi (SimBanking) na kuepuka usumbufu wa kufuata huduma katika matawi.

Sitta pia aliongeza kuwa ‘Transact by Finger’ inamaanisha kwamba mteja wa CRDB anaweza kupata huduma zote za kifedha ikiwemo kufanya malipo ya aina mbalimbali hivyo awamu ya pili ya kampeni hiyo inalenga kuhakikisha wafanyakazi wanawaelimisha wateja umuhimu wa huduma hiyo.

"Kupitia SimBanking, mteja anaweza kufanya mihamala hadi millioni 20 kwa siku, tukiwaelekeza namna ya kutumia huduma hiyo, tutapunguza msongamano kwenye matawi yetu" alisema Sitta.

Naye Meneja Uhusiano CRDB Kanda ya Ziwa, Erasto Alfred alisema kupitia kampeni hiyo, wateja na wafanyakazi wanayo fursa ya kujishindia zawadi mbalimbali baada ya kutumia huduma ya SimBanking.

Kwa upande wake Meneja wa CRDB Tawi la Mwaloni jijini Mwanza, Munira Nasro alisema matawi yote ya benki hiyo yamejipanga kuwahudumia kwa weledi wateja na kuhakikisha wanajiunga na huduma ya SimBanking ili kwa pamoja wafurahie huduma za kifedha kwa urahisi na haraka.

Awamu ya kwanza ya kampeni ya Transact By Finger ilizinduliwa Machi 04, 2024 na kudumu kwa muda wa miezi mitatu ambapo awamu ya pili itafikia tamati Disemba 2024.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akizungumza na wafanyakazi wa benki ya CRDB jijini Mwanza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Transact By Finger, Road to December.
Naye Meneja Uhusiano CRDB Kanda ya Ziwa, Erasto Alfred akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mameneja na wafanyakazi wa CRDB jijini Mwanza wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Transact By Finger, Road To December.
Mameneja na wafanyakazi wa CRDB jijini Mwanza wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya Transact By Finger, Road To December.
Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mameneja na wafanyakazi wa benki hiyo jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.