LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge wa Kishapu kuendeleza michezo kwa vijana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Boniphace Butondo.
Diwani wa Kata ya Kishapu mkoani Shinyanga, Joel Ndettoson.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Joseph Mkude.
Timu ya Bodaboda FC ya Kishapu mkoani Shinyanga imeibuka na ubingwa wa mshindi wa kwanza kwa bao la goli 1:0 dhidi ya Fama FC ya Igaga katika ligi ya Butondo Kishapu Shagy Cup na kuondoka na kitita cha Tsh. 1,500,000/=.

Akizungumza Julai 06,2024 kwenye kilele cha ligi hiyo, mbunge wa jimbo la Kishapu, Boniphace Butondo aliahidi kuendeleza michezo jimboni humo kupitia ligi hiyo.

Aliwapongeza washindi wa kwanza Bodaboda FC Kishapu, washindi wa pili Fama FC na washindi wa tatu Ngundangali FC.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude alizipongeza timu zote zilizoshiriki na kusema kuwa ligi hiyo imewaweka pamoja vijana.
Na Sumai Salum, Kishapu

No comments:

Powered by Blogger.