LIVE STREAM ADS

Header Ads

Upasuaji wa kwanza wafanyika kwa mafanikio Gumanga wilayani Mkalama

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kituo cha Afya cha Gumanga kilichopo kata ya Gumanga Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kimefanikiwa kufanya upasuajia mkubwa wa kwanza wa dharura kwa mama mjamzito toka kufunguliwa kwake.

Akizungumza mara baada ya upasuaji huo, Mganga Mkuu wilaya ya Mkalama, Dkt. Solomon Michael amesema upasuaji huo umefanyika Julai 01,2024 chini ya madaktari wawili wakisaidiwa na wauguzi pamoja na mtalaamu wa usingizi.

"Kwa mara ya kwanza tumefanikiwa kufanya upasuaji mkubwa hapa Gumanga toka tuanzishe huduma hizi za upasuaji. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu. Mtoto aliyezaliwa ni wa kike na uzito wa kilo 3.1, hali ya mama na mtoto inaendelea vizuri" aliongeza Dkt. Michael.

Kwa mujibu wa Dkt. Solomon Michael alisema mjamzito huyo amefika kituoni hapo siku ya Jumatatu ya Julai 1,2024 muda wa asubuhi na kufanyiwa upasuaji muda wa saa moja usiku.

Aidha timu ya wataalamu iliyoongoza zoezi hilo ni Dkt. Sira Laurent Kisamhara, akisaidiwa na Dkt. Lazaro Chambo, wauguzi wakiwa Seleman Mwalukasa, Faraja Shadrack, na Richard Sopeter mtaalamu wa usingzi pamoja a mtaalam wa Maabara Patric Sanga

Kituo cha afya cha Gumanga kinakuwa ni kituo cha tatu cha Serikali wilayani Mkalama kinachotoa huduma za upasuaji, vingine ni Hosipitali ya Wilaya ya Mkalama pamoja na kituo cha Afya cha Kinyambuli.

No comments:

Powered by Blogger.