Dkt. Biteko ahimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com

Dkt. Biteko ametoa rai hiyo Julai 29,2024 mkoani Rukwa wakati wa kuweka jiwe la msingi la mradi wa kusafirishia umeme kilovoti 400 kutoka mkoani Iringa, Mbeya na Sumbawanga (Rukwa) katika hafla iliofanyika viwanja vya Kata ya Malangali ambapo mradi huo unagharimu shilingi bilioni 517.
‘’Tutaangalia namna ya kupata fedha kwa jili ya kuongeza mfuko wa nishati safi ya kupikia ili Watanzania waweze kupata Nishati safi ya kupikia’’ amesema Dkt. Biteko.
Naye Balozi wa Mtu Ni Afya, msanii Mrisho Mpoto amesema anaiomba jamii ifanye kweli katika kutumia nishati safi ya kupikia na wananchi wasibaki nyuma kuhamia kwenye nishati hiyo ikiwemo gesi.
Amesema ni wakati sasa watu waachane na nishati chafu ya kupikia ikiwemo kuni ama mkaa.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko (katikati) akiwa na Mkuu wa Mkoa Rukwa, Charles Makongoro (kulia) na kiongozi wa CCM (kushoto).
Msanii, Mrisho Mpoto ambaye ni balozi wa kampeni ya Mtu ni Afya.
No comments: