LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Misungwi ahamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi Pamba Day

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mashabiki wa soka mkoani Mwanza wameendelea kuhamasika kuelekea siku ya Pamba Jiji FC (Pamba Day) itakayofanyika Agosti 10, 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba.

Mashabiki hao wameendelea kununua tiketi kwa ajili ya tamasha pa Pamba Day na kufungua matawi ya timu hiyo katika maeneo yao ambapo tayari matawi yamefunguliwa katika Wilaya za Ukerewe, Kwimba, Magu na Misungwi.

Akifungua tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC tarehe 30 Julai 2024, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi aliwahimiza mashabiki kuendelea kununua tiketi za Pamba Day akissema wataandaa usafiri utakaowafikisha mashabiki CCM Kirumba kuipa hamasa timu yao.

Pia Samizi alinunua jezi 10 za timu ya Pamba Jiji FC na kuzigawa kwa mashabiki kama sehemu ya kutoa hamasa kuelekea tamasha la Pamba Day.

Mjumbe wa Kamati ya Hamasa ya Pamba Jiji FC, Agnes Magubu ambaye pia ni Afisa Utamaduni Halmashauri ya Jiji la Mwanza alisema hamsa imekuwa kubwa na wana Mwanza wameipokea vyema timu hiyo baada ya kurejea tena ligi kuu msimu wa mwaka huu 2024/25.

Mashabiki wilayani Misungwi wamesisitiza timu hiyo kujipanga ili kufanya vizuri katika ligi kuu na kurejesha heshima yake kama awali na si kuwa timu inayofungwa ovyo na kila timu ligi kuu.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC mjini Misungwi. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Hamasa ya Pamba Jiji FC, Agnes Magubu.

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC mjini Misungwi.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi (kushoto) akifurahia uzinduzi wa tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC mjini Misungwi. Kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Hamasa ya Pamba Jiji FC, Agnes Magubu.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Johari Samizi akiwa na mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC.
Afisa Michezo Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mohamed Bitegeko akihamasisha mashabiki wilayani Misungwi kununua tiketi ili kushiriki tamasha la Pamba Day.
Mjumbe wa Kamati ya Hamasa ya Pamba Jiji FC, Agnes Magubu akizungumza kwenye hamasa ya Pamba Day wilayani Misungwi.
Wajumbe wa kamati ya hamasa ya Pamba Day wakiwa kwenye picha ya pamoja na mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC wilayani Misungwi.
Wajumbe wa kamati ya hamasa ya Pamba Day wakiwa kwenye picha ya pamoja na mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC wilayani Misungwi.
Mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC wilayani Misungwi wakiwa kwenye shangwe la kuuza tiketi na jezi kuelekea tamasha la Pamba Day tarehe 10 Agosti 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba.

No comments:

Powered by Blogger.