Katibu Mkuu Zanzibar atimiza ahadi yake kwa wana Simba, Yanga
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeida Rashid Abdallah ametimiza ahadi yake kwa mashabiki wa timu za Simba SC na Yanga SC kutoka Kijiji cha Nyang'hanga, Wilaya ya Magu mkoani Mwanza, aliyoitoa Julai 04,2024 alipofanya ziara ya kimafunzo kijijini hapo kupitia shirika la KIVULINI.
Katibu Mkuu huo aliahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa kila tawi kwa ajili ya kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa ofisi baada ya mashabiki hao kugeuza utani wao wa jadi katika kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake na watoto pamoja na kusaidia kwenye shida na raha.
Hatua hiyo ni baada ya kujengewa uwezo na shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI wakati linatekeleza mradi wa kudhibiti matukio ya ukatili wa kijinsia wilayani Magu ambapo Kijiji cha Nyang'hanga kilichopo Kata ya Sukuma ni miongoni mwa maeneo yaliyofikiwa na mradi huo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto), akimkabidhi Msemaji wa mashabiki wa timu ya Simba SC tawi la Nyang'hanga Kata ya Sukuma wilayani Magu, Amos Say (kulia) shilingi laki tano zilizotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeida Rashid Abdallah ili kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa ofisi.
Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa mashabiki wa timu ya Yanga SC tawi la Nyang'hanga Kata ya Sukuma wilayani Magu, Mashaka Bukumbi (kushoto) shilingi laki tano zilizotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abeida Rashid Abdallah ili kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa ofisi.
Mashabiki wa timu ya Simba SC tawi la Nyang'hanga Kata ya Sukuma wilayani Magu, mkoani Mwanza.
Mashabiki wa timu ya Yanga SC tawi la Nyang'hanga Kata ya Sukuma wilayani Magu, mkoani Mwanza.
Wanawake wa kikundi cha Masalagula kilichopo Nyang'hanga wilayani Magu wakitumbuiza.
TazamaBMG TV hapa chini
PIA>>> Bonyeza hapa kusoma zaidi
No comments: