LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau jijini Mwanza watoa maoni Dira 2050

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wadau wa maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza wameishauri Serikali kuboresha mfumo wa elimu utakaosaidia kukidhi mahitaji ya soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Wadau hao kutoka makundi mbalimbali ya kijamii wametoa ushauri huo Agosti 16, 2024 wakati wakitoa maoni yao namna ya kuboresha Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025/2050

Miongoni mwa maboresho ya mfumo wa elimu yaliyopendekezwa ni pamoja na kufundishwa kwa elimu ya sheria katika ngazi zote za elimu ili kuwezesha watanzania kutambua haki na wajibu wao ikiwemo kutokuwa wahanga wa kuvunja sheria za nchi.
Elimu ya Tehama pia imependekezwa kufundishwa katika ngazi zote za elimu ili kuwezesha wahitimu kujiajiri kupitia fursa zinazopatikana kupitia uchumi wa kidigitali.

Mapendekezo mengine ni Serikali kuruhusu maarifa kugeuzwa kuwa mali kwa wanafunzi wenye vipaji vikiwemo vya uigizaji kuendelezwa badala ya kulazimishwa kujifunza kujifunza taaluma nyinginezo tofauti na vipaji vyao.

Aidha mfumo wa elimu kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu umependekezwa kutumia lugha zote mbili za Kiswahili na Kiingereza ili kuwezesha watanzania kumudu ushindani kwenye nyanja mbalimbali zilizoko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na duniani kwa ujumla.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Nyamagana, Peter Begga ameshauri kuongezwa kwa nafasi za ubunge wa kuteuliwa na Rais ili kuwezesha makundi mbalimbali ikiwemo vijana,watu wenye ulemavu,wazee,vyama vya siasa pamoja na wamachinga kunufaika na nafasi hizo kupitia uteuzi wa wawakilishi wao.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Tawala Wilaya Nyamagana, Thomas Salala amesema Dira ya Taifa ya Maendeleo ni muhimu kutokana na kubeba dhima namna Taifa linavyopaswa kuwa na hivyo kuwaasa wananchi kuendeleo kutoa maoni yatakayowezesha kupatikana kwa Dira ya Taifa kwa miaka 25 ijayo.
Katibu Tawala Wilaya Nyamagana, Thomas Salala.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.