LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mashabiki wa Simba SC Singida watoa msaada kwa wahitaji

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mashabiki wa Simba Mkalama mkoani Singida, Agosti 03,2024 wameadhimisha Simba Day kwa kutoa msaada katika hospitali ya Wilaya pamoja na shule ya Sekondari Nduguti.

Kiongozi wa mashabiki wa Simba wilayani Mkalama, Tesha Daniel amewaomba wananchi Mkalama kuwa na tabia ya kujitolea katika matukio ya kijamii kwa kutoa msaada mbalimbali kwa watu wenye uhutaji kwa lengo la kujenga jamii yenye upendo na amani.

"Tuifanye dunia kuwa sehemu salama, tunawajibu wa kujitolea pale inapobidi kwa ajilii ya kuleta tabasamu kwa ndugu zetu, niwaombe tuwe na desturi kama hii ya kuitika pale tunapoitwa kwa ajili ya wengine" amesema Tesha.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Nduguti, Rosemary Richard ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha Nne amewashukuru mashabiki wa Simba kwa upendo wao na kuwaomba wananchi wilayani Mkalama kuiga mfano wa mashabiki hao wa Simba.

Vifaa vilivyotolewa na mashabiki wa Simba SC katika wodi ya wazazi ya hospitali ya Wilaya ni pamoja na Sabuni, sukari na kwa upande wa shule ya Sekondari Nduguti ni taulo za kike kwa wanafunzi wakike na sabuni kwa wanafunzi wa kiume

No comments:

Powered by Blogger.