DC Nyamagana aongoza hamasa kuelekea Pamba Day
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mbio hizo zimefanyika Jumamosi Agosti 03,2024 katika mitaa ya Jiji la Mwanza na kushirikisha klabu mbalimbali za jogging, mashabiki na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza.
Makilagi ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi mkoani Mwanza kuendelea kununua tiketi ili kwenda kuipa hamasa timu ya Pamba Jiji FC ambayo itacheza na Vitalo kutoka Burundi.
Matukio mengine ni kutoa mahitaji katika shule ya wanafunzi maalum Buhongwa na kufungua tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC Buhongwa.
Jogging ikiendelea uwanja wa Nyamagana.
Bodaboda jijini wakiwa kwenye hamasa kuelekea Pamba Day Agosti 10, 2024 uwanja wa CCM Kirumba.
Hamasa kuelekea Pamba Day ikifanyika kwenye mitaa ya Jiji la Mwanza.
Pamba Jiji FC, Mbele- Mbele Zaidi Yao #UtapigwaKamaUtakavyokuja.
No comments: