LIVE STREAM ADS

Header Ads

Pamba Jiji FC yakabidhi msaada kwa wenye mahitaji maalumu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya hamasa ya Pamba Day ikiongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala imekabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika Shuke ya Msingi Buhongwa.

Salala amesema hatua hiyo ni sehemu ya matendo ya huruma ikiwa ni sehemu ya matukio muhimu ya hamasa kuelekea Siku ya Pamba (Pamba Day) itakayofanyika Agosti 10,2024 CCM Kirumba.

Wakitoa shukurani baada ya kupokea mahitaji hayo, Mwalimu Rehema Kagembe na mwanafunzi
Shamim Abdallah wameiombea baraka timu ya Pamba Jiji FC wakisema hatua ya kuwakumbuka wenye mahitaji maalumu itachagiza ushindi wao kwenye ligi kuu msimu wa mwaka 2024/25.

Matukio mbalimbali yameendelea kufanyika mkoani Mwanza ikiwemo uzinduzi wa mashina ya mashabiki wa Pamba Jiji FC, kuuza tiketi na jezi kuendelea kilele cha 'Pamba Day' Agosti 10, 2024 uwanja wa CCM Kirumba.

Pamba Jiji FC wanasema 'Mbele, Mbele Yao Zaidi' na 'Utakpigwa Kama Utakavyokuja'.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mwalimu wa wanafunzi maalumu shule ya msingi Buhongwa, Mwl. Rehema Kagembe (kulia) na mwanafunzi Shamim Abdallah (kushoto) wakitoa shukurani kwa niaba ya wenzao baada ya kupokea mahitaji mbalimbali kutoka Kamati ya hamasa ya Pamba Jiji FC.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Buhongwa.
Kamati ya hamasa ya Pamba Jiji FC imekabidhi bidhaa mbalimbali ikiwemo taulo za kike, madaftari, kalamu, sabuni vinywaji na viburudisho mbalimbali kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu katika shule ya msingi Buhongwa jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.