Tawi la mashabiki wa Pamba Jiji FC Buhongwa lazinduliwa
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana, Thomas Salala amezindua tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC lililopo Buhongwa jijini Mwanza.
Salala amezindua tawi hilo Jumamosi Agosti 03, 2024 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Hamasa ya Siku ya Pamba (Pamba Day) itakayofanyika Agosti 10, 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba.
"Ili Pamba Jiji FC ifanye vizuri, lazima kuiunga mkono kwa kununua tiketi na jezi itakapokuwa inacheza. Pia tujitokeze kwa wingi Pamba Day kuishangilia itakapokuwa inacheza na timu ya Vitalo kutoka Burundi" amesema Salala.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala akipandisha bendera ya Pamba Jiji FC wakati wa uzinduzi wa tawi la mashabiki wa timu hiyo, Buhongwa jijini Mwanza.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala akizungumza kwenye uzinduzi wa tawi hilo. Kushoto ni Afisa Utamaduni Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Agnes Magubu na kulia ni Afisa Habari Pamba Jiji FC, Martin Sawema.
Utapigwa Kama Utakavyokuja. Ukija kwa heshima, unapigwa goli chache na ukija kwa mbwembwe, unapigwa goli za kutosha.
Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala akizindua tawi la mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC eneo la Buhongwa jijini Mwanza.
Zoezi la kuzindua matawi ya mashabiki wa timu ya Pamba Jiji FC tayari limefanyika Ukerewe, Kwimba, Magu, Misungwi, Sengerema na Nyamagana.
No comments: