LIVE STREAM ADS

Header Ads

Manguruwe atunukiwa udaktari wa heshima

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mfugaji maarufu wa nguruwe na mmiliki wa mradi wa Kijiji cha Nguruwe Zamahero Dodoma, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa mitandaoni, Mr. Mangurue ameutunukiwa shahada ya udhamiri wa falsafa ya biashara na maendeleo ya jamii (Doctor in Business and Humanity) ya chuo Kikuu cha African Graduate University.

Ametukuniwa udaktari huo baada ya kuongoza vizuri biashara zake,kusaidia wengine na kuwa na falsafa ya kuamini na kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kufikia malengo makubwa na kufundisha na kuhamasisha wengine kwa maendeleo ya nchi.

Digrii hiyo ya udhamiri imetolewa na Professor Stephen Nzowa na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wawekezaji katika mradi wake, ndugu, jamaa na marafiki zake kutoka ndani na nje ya nchi.

Mr. Manguruwe kwa sasa Dk. Manguruwe ameeleza furaha yake baada ya kutunukia udaktari huo, amemshukuru Mwenyezi Mungu na mke wake Rose Simon Mnkondya kwa kuwa naye bega kwa bega ili kutimiza kazi zake vizuri na kuweza kutunukiwa Udaktari wa Falsafa ya Biashara na Maendeleo ya Jamii.

No comments:

Powered by Blogger.