Waziri Mavunde aipongeza CRDB kwa kuwakopesha wachimbaji madini
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama mkoani Shinyanga.

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo kilichofanyika Agosti 19,2024 Mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.
***
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Benki ya CRDB kwa kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wachimbaji wakiwamo wadogo na kuyataka mabenki na taasisi nyingine za fedha kuiga mfano huo.
Waziri Mavunde alitoa kauli hiyo Jumatatu Agosti 19,2024 mjini Kahama alipokabidhiwa ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa utoaji huduma za fedha kwa wachimbaji wadogo na wa kati kutokana na maelekezo aliyoyatoa mwaka 2023 alipokutana na Wachimbaji wa madini, viongozi wa serikali, wafanyakazi wa Benki ya CRDB na wadau mbalimbali wa sekta ya madini.
Katika hafla hiyo, Waziri Mavunde pia alikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.
“Wachimbaji wadogo ni jeshi kubwa kwenye sekta ya madini nchini lakini lenye changamoto ya mtaji. Iwapo benki zetu za ndani zitawapa kipaumbele watu hawa kama mnavyofanya Benki ya CRDB, mchango wa sekta ya madini kwenye pato letu la taifa utaongezeka kwa kiasi kikubwa. Nawapongeza Benki ya CRDB kwa kuuona umuhimu wa kuizingatia sekta hii” alisema Waziri Mavunde.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo.
"Leo nasimama hapa kwa furaha kubwa kuwashukuru na kuipongeza Benki ya CRDB kuwa kati ya benki chache za mfano ambazo zimeamua kuja kuwawezesha na kuwainua wachimbaji, watoa huduma. Nataka niwaambie CRDB hamjapoteza, mmeingia kwenye njia sahihi. Hili eneo mlilisahau,wachimbaji wenyewe wanakopeshana, hivyo naomba taasisi za kifedha zitambue kuwa wachimbaji wanakopesheka, wana uwezo wa kulipa na mtayaona mafanikio ndani ya muda mfupi kupitia hii sekta ya madini.
CRDB niwapongeze sana, kiasi shilingi Bilioni 64 mlichotoa kwa wachimbaji wa madini siyo kiasi kidogo, kinakwenda kuchochea uchumi wa sekta ya madini, kinakwenda kubadilisha maisha ya wachimbaji wadogo nchini. Hii ni nyenzo ya kuchochea sekta ya madini, CRDB hamjapotea mumewekeza sehemu sahihi na nitoe rai kwa taasisi zingine za kifedha na benki zingine kuiamini sekta ya madini" alisema Mavunde.
Mwaka jana, Waziri Mavunde aliwaeleza watendaji wa benki nchini juu ya changamoto ya upatikanaji wa huduma za fedha ikiwamo mikopo kwa wachimbaji wadogo na kuwataka kuangalia namna ya kurahisisha upatikanaji wake ili kukuza mchango wa sekta ya madini nchini ambayo inaajiri maelfu ya wananchi katika mikoa mbalimbali nchini.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
Katika hafla hiyo, Waziri Mavunde alisema Serikali itandelea kuimarisha mazingira ya uchimbaji nchini ikiwemo kujenga uwezo wa wachimbaji wadogo kufanya utafiti utakaowasaidia kuchimba maeneo yenye uhakika wa kupaa madini tofauti na hali ilivyo sasa wanapochimba kwa kubahatisha.
Mavunde alisema Serikali inaendelea na juhudi za kuwawezesha wachimbaji wadogo kwa kutekeleza mikakati tofauti kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kwa kuwa inatambua kuwa bado wachimbaji wadogo wengi wanafanya shughuli zao bila kufanya utafiti wa kisayansi hivyo kutokuwa na uhakika wa kupata madini wanayoyakusudia.
Waziri Mavunde alisema hayo baada ya Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa kumjulisha kuhusu hatua kadhaa zilizofanywa na benki katika kuwawezesha wachimbaji wadogo pamoja na changamoto ilizokutana nazo.
Akiainisha mchango wa Benki ya CRDB, Raballa alisema imeanzisha kitengo maalum cha madini ili kutoa wigo mpana wa utekelezaji wa mikakati inayoelekezwa kwenye sekta ya madini na kujenga uwezo kwa wafanyakazi kuchambua maombi na mahitaji ya wachimbaji wadogo wa madini.
Kitengo hiki, Raballa alisema kinasaidia kuratibu utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kwa wachimbaji wadogo ambayo wanaipata kwa wakati unaostahili, benki inawapa huduma za bima, inafadhili ununuzi na uingizaji wa kemikali pamoja na mitambo muhimu ya uchakataji na uchenjuaji madini nchini na inawasaidia kubadili fedha za kigeni kila inapohitajika.
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
“Benki yetu imeendelea kuwa mstari wa mbele kufanikisha upatikanaji wa fedha za uwekezaji wa miradi ya madini kuanzia kwa wachimbaji wadogo mpaka wakubwa. Hadi sasa tumeshakopesha zaidi ya shilingi bilioni 64. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 19 zimetolewa kwa wachimbaji wadogo” alisema Raballa.
Kwa wachimbaji wakubwa, afisa huyo alisema Benki ya CRDB imeidhinisha mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 120 kwenye mradi wa uchimbaji wa madini ya kinywe unaotekelezwa na kampuni ya Faru Graphite na imeteuliwa kuongoza jopo la mabenki kutafuta fedha za ujenzi wa mradi uchimbaji wa madini ya urani utakaogharimu dola milioni 900 za Marekani baada ya kuthibitishwa na Tume ya Madini.
“Benki yetu pia imeanzisha kitengo maalumu kinachosimamia mnyororo wa thamani ambacho moja ya majukumu yake ni kuwaunganisha watu na fursa zilizopo kwa kuhakikisha kinaboresha mahusiano na huduma zetu kuwafikia hadi wateja kwa wakati sahihi. Hata hivyo, kati ya changamoto kubwa zilizopo ni wachimbaji wadogo kutotunza kumbukumbu za uzalishaji na mauzo ya madini jambo linaloweza kuwaongezea vigezo vya kupata mikopo kwa urahisi” alisema Raballa.
Wadau wa Sekta ya Madini wakiwa kwenye kikao.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony Mavunde akizungumza wakati wa kikao cha kupokea ripoti ya Benki ya CRDB katika utekelezaji wa kutoa huduma za kifedha kwa wachimbaji wa kati na wadogo.
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa.
Waziri wa Madini, Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa.
Waziri wa Madini, Mheshimiwa Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.
Waziri wa Madini, Anthony (mwenye tai nyekundu kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Bilioni 10 kwa baadhi ya wachimbaji wa Kanda ya Ziwa itakayotumika kuimarisha shughuli zao kwenye maeneo tofauti wanakotoka.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini nchini (FEMATA), John Bina.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini nchini (FEMATA), John Bina.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha.
Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini, Masanche Kasaka.
Mbunge wa Jimbo la Nyang'wale, Hussein Kassu.
Mbunge wa Jimbo la Msalala, Iddi Kassim.
Kamishna wa Madini nchini, Dkt. Abdulrahman Mwanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Mboni Mhita.
Meneja Mwandamizi wa Dawati Maalumu la Madini la Benki ya CRDB, Abdulrahim Msonde.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Wadogo na wa kati wa Benki ya CRDB, Agness Kisinini.
Wadau wa sekta ya madini.
Wadau wa sekta ya madini.
Wadau.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (mwenye suti ya bluu) akiangalia kikundi cha burudani ya ngoma ya utamaduni ya kabila la wasukuma.
No comments: