LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Njombe wakubali kufanya kweli, kuwa na vyoo bora

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Wakazi wa Mkoa wa Njombe wameamua kufanya kweli ili kuhakikisha wanaachana na matumizi ya vyoo vya zamani kwa kujenga vyoo vya kisasa.

Akizungumza wakati wa mkutano uliofanyika katika Kata ya Iwawa, mmoja wa wakazi wa kata hiyo Tumwanyuke Ngakonda aliwashauri wananchi kuendelea kufanya kweli kwa kujenga vyoo vya kisasa na kuacha na vile vyoo vya zamani vilivyokuwa vinatumia nyasi.

“Tufanye kweli kwa kuweza kujenga vyoo vya kisasa vyenye milango na kuweka sehemu ya kunawia mikono na maji tiririka hii itasaidia sana katika kuweza kuepuka magonjwa’’ alisema.
Naye Mkazi wa Makete mjini, Anna Mwajeka alisema yeye ameamua kufanya kweli kwa kujenga choo chake cha kisasa chenye ubora.

Alisema katika utunzaji wa mazingira pia amekata kubaki nyuma kwa kujijengea utaratibu malumu wa kufanya usafi wa mazingira kwa lengo la kuepusha usambaji ovyo wa takataka.

Naye Mama lishe kutoka Kata Iwawa,Scola Atilio alisema usafi unatakiwa kuanzia nyumbani mpaka kazini au maeneo ya biashara.

‘’Usafi unaanzia na sisi wenyewe kwa mfano sisi mama lishe tukifanya kweli tutakuwa tumeimarisha suala zima la afya. Tuwe na sehemu malumu ya kuhifadhi takataka’’ alisema.

No comments:

Powered by Blogger.