UVDS wafanya usafi CCM Kirumba kuelekea Pamba Day
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Kuelekea Pamba Day kesho jumamosi Agosti 10, 2024, Chama cha Makondakta na Wasaidizi Wao jijini Mwanza (UVDS), kimefanya usafi katika uwanja wa CCM Kirumba.
Mwenyekiti wa UVDS, Mlimi Juma ameahidi wanachama wa chama hicho kujitokeza pia kwa wingi kuishangilia timu ya Pamba Jiji FC siku ya kesho na kwenye mechi za ligi kuu.
Tamasha la siku ya Pamba Jiji FC (Pamba Day) litajumuisha burudani mbalimbali ikiwemo mchezo wa kirafiki dhidi ya Vitalo kutoka Burundi.
Mwenyekiti wa UVDS Mkoa Mwanza, Mlimi Juma akieleza namna chama hicho kimekuwa na utaratibu wa kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo kufanya usafi kila mwisho wa mwezi katika mitaa mbalimbali na maeneo ya umma.
Mwenyekiti wa UVDS Mkoa Mwanza, Mlimi Juma akigawa vipeperushi vya hamasa ya Pamba Pamba ili makondakta nao wakavigawe kwenye vituo vya daladala.
PIA>>> BONYEZA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments: