LIVE STREAM ADS

Header Ads

APOT waendesha uchunguzi kwa wenye ulemavu wa viungo Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Wataalamu wa Viungo Bandia na Vifaa Tiba Saidizi Tanzania (Association of Prosthetists and Orthotists of Tanzania- APOT), kimeendesha kambi ya uchunguzi wa kubaini watu wenye ulemavu wa viungo jijini Mwanza ili kuwasaidia kupata viungo bandia.

Kambi hiyo imefanyika Jumatatu Septemba 02, 2024 katika uwanja wa Furahisha ikiwa ni jitihada za chama hicho kwa kushirikiana na wadau, kuwasaidia watu wenye ulemavu wa viungo wasijimudu kiuchumi kupata viungo bandia hatua itakayowasaidia shughuli za uzalishaji mali.

Katibu wa APOT, Lilian Mrisha amesema APOT imelenga kuboresha upatikanaji huduma za tiba ya viungo kwa wananchi kwa kuendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu wa viungo na kuanzisha vituo vya tiba katika mikoa mbalimbali nchini.

Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Kusirie Swai ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wananchi kuchukua tahadhari na kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambiza ikiwemo kisukari, kansa, mfumo wa damu na ajali kwani yamekuwa sababu kuu zinazochangia ongezeko la ulemavu katika jamii.

Mmoja wa wakazi wa Mwanza, Dotto Mlesi ambaye ni miongoni mwa wenye ulemavu waliojitokeza kwenye kambi hiyo ya uchunguzi wa viungo ametoa rai kwa APOT kuendelea kusaidia upatikanaji wa viuongo bandia kwa wahitaji wengine.

Kambi hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya shughuli mbalimbali za chama hicho katika kuelekea kwenye mkutano wake mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Mwanza ambapo viungo bandia vitakabidhiwa kwa wahitaji waliobainika kwenye uchunguzi huo.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Kusirie Swai akizungumza kwenye kami ya uchunguzi bure kwa wananchi wenye ulemavu wa viungo jijini Mwanza.
Katibu wa APOT, Lilian Mrisha (kushoto) akimkaidhi Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Kusirie Swai (kulia) risala ya chama hicho wakati wa kambi ya uchunguzi kwa watu wenye ulemavu wa viungo.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kambi hiyo, Dkt. Bago Juma akizungumza wakati wa kambi ya uchunguzi kwa wenye ulemavu wa viungo ambapo amewashukuru wadau wote waliogharamia upatikanaji wa viungo bandia ambapo ametumia fursa hiyo kuwasihi wadau kuendelea kusaidia kwani uhitaji ni mkubwa.
Dkt. Claude Mushi kutoka Kliniki ya Tiba ya Viungo Mwanza (kushoto) akifanya uchunguzi kwa mmoja wa wananchi waliojitokeza kwenye kambi ya uchunguzi wa viungo iliyoanyika uwanja wa Furahisha.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Kusirie Swai (kushoto) akiwa kwenye banda la Kliniki ya Tiba ya Viungo Mwanza wakati wa kambi ya uchunguzi wa viungo kwa wenye ulemavu iliyoandaliwa na APOT.
Mwonekano wa baadhi ya viungo bandia.
Sajenti Ninga Gilagiza kutoka jeshi la polisi kitengo cha elimu ya usalama barabarani Mkoa Mwanza akitoa elimu kwa wananchi ili kuchukua tahadhari ya kujikinga na ajali zinazoweza kusababisha wapate ulemavu.
Sajenti Ally Yateri kutoka jeshi la polisi kitengo cha elimu ya usalama barabarani Mkoa Mwanza akitoa elimu kwa wananchi ili kuchukua tahadhari ya kujikinga na ajali zinazoweza kusababisha wapate ulemavu.
Picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.